• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPC yavutia Vyama vya siasa Afrika vyakubaliana kujikita katika maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-07-24 08:54:04

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    MKUTANO wa kihistoria ulioandaliwa na Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania ulioshirikisha vyama vya siasa Afrika zaidi ya 40, umemalizika kwa mafanikio makubwa.

    Mkutano huo, uliofanyika kwa siku mbili, pamoja na mambo mengine viongozi wa vyama hivyo wamekubalina kuhakikisha vyama vya siasa vinajikita katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuachana na masuala ya nadharia.

    Pia, vyama hivyo kwa kufuata mfano wa Chama cha CPC kilichotawala nchi hiyo tangu mwaka 1949 na katika utawala wake imeangalia zaidi maendeleo ya watu wake kwa kutekeleza ujamaa wa kichina ambao unatekelezwa kwa kutumia mazingira ya nchi hiyo.

    Bila kuteteleka na masuala ya kwenda na wakati, nchi hiyo yenye wananchi zaidi ya bilioni mbili imejikita katika ujamaa wenye kuangalia mazingira ya nchi yao.

    Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bashiru Ally anasema katika mkutano huo wa kwanza kufanyika Afrika umefanyika kwa mafanikio kwa vyama vya siasa Afrika kuamua kuachana na kuomba kura.

    Anasema wamekubaliana vyama vya siasa kuwa wamekuwa wakifanya makosa kugeuza vyama kutafuta kura badala ya kuwa hazina ya kuandaa mipango kwa maendeleo ya watu na kusimamia misingi ya maendeleo.

    "Sifa ya CPC ni kujenga uchumi na jamii iliyo huru kwa hiyo tumekubaliana kuimarisha vyama vyetu kwani baba wa taifa hayati Julius Nyerere alisema bora umasikini mwingine kuliko wa fikra"anasema.

    Anasema hatua hiyo itasaidia kuachana na kunyonywa ,kudhalilishwa na kudharauliwa na wale ambao wametutawala kwani kazi ya kupambana na ukoloni haijaisha kwa sasa imemalizika ile ya ukoloni kisiasa kwa sasa ni kupambana ili rasilimali zisiporwe.

    Mkutano huo uliohudhuliwa na Mkuu wa idara ya mahusiano ya kimataifa na waziri wa Mahusiano ya kitaifa wa CPC song Tao na Naibu Waziri wa Mahusiano ya kimataifa wa CPC Xu Luping na wajumbe mbalimbali wa chama hicho .

    Magufuli anashukuru CPC kwa kuchagua CCM kuwa mwenyeji wa mkutano huo.

    Anabainisha kuwa ukongwe wa CCM katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika huku ikikaa madarakani kwa zaidi ya miaka 55 inatoa mwenendo wa vyama vingi kujifunza katika chama hicho.

    Magufuli katika ufunguzi wa mkutano huo anabainisha sababu ya nchi za Afrika kuendelea kushirikiana na china kwa kuwa uhusiano uliodumu kwa muda mrefu umejengwa katika misingi ya kuheshimiana na kuelewana.

    Mkutano huo wa kwanza kufanyika barani aFrika lakini wa pili duniani baada wa awali kufanyika desemba mwaka jana,Beijing China.

    Anaeleza mahusiano baina ya pande hizo mbili umejikita katika Nyanja mbalimbali za kibiashara, uwekezaji, kilimo, Elimu, Sayansi na Teknolojia.

    Anasema mahusiano hayo yameimarika kutokana na China kutoa misaada isiyokuwa na masharti lakini ikijikita katika maelewano maelewano kwa kujenga misingi ya kuheshimiana na kuelewana.

    Anasema mbali ya misaada mbalimbali inayotolewa na China katika nchi za Afrika bado kuna fursa nyingi za kukuza na kuimarisha ushirikiano katika kukuza biashara.

    Huku akitaka nchi za Afrika kutumia vema idadi ya watu nchini China kwa kupanua soko la bidhaa kwa kuuza bidhaa mbalimbali katika kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya pande hizo.

    Anatoa mfano wa biashara ya kahawa kuwa katika watu bilioni 2.3 nchini China wanaweza kila mmoja kunywa kikombe kimoja hivyo kupata biashara kubwa.

    Anataja fursa nyingine ambazo zinaweza kutumika nchini China ni Pamba au Chai huku wachina kufika kuangalia vivutio vya utalii ambavyo ni vingi na vya pili duniani ikitanguliwa na Brazil.

    Anasema soko la Afrika nchini China linahitaji kupanuliwa kwa kuuza bidhaa pamoja na China kuongeza uwekezaji Afrika hususan katika kilimo viwanda, madini na mengineyo.

    Anasema ushirikiano baina ya pande hizo mbili umefikia kiwango cha juu kwa kujenga misingi ya kuheshimiana na kuelewana jambo ambalo misaada ya China katika nchi za Afrika haiambatani na masharti mengi.

    "Hili ndiyo haswa nchi za Afrika tunataka, kwani hatuhitaji masharti bali tunahitaji maelewano, ushirikiano ambayo itanufaisha wote, tunashukuru Wachina kwa kuheshimu misingi hiyo'anasema

    Anasema kwa sasa nchi za Afrika ziko katika kujikomboa kiuchumi na Tanzania imedhamiria kuongoza mapambano hayo.

    Anasema miaka ya 2000 Afrika na China walianzisha jukwaa la Ushirikiano (FOCAC)ambalo mikutano yake hufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa kuweka misingi rasmi ya ushirikiano na mkutano wa saba utafanyika Septemba mwaka huu Beijing China.

    Alisema kutokana na kuanzishwa kwa ushirikiano huo,kumepatikana mafanikio katika Nyanja mbalimbali kama biashara kuongezeka toka dola za marekani bilioni kumi na sasa inakadiliwa kufikia dola bilioni 200 huku uwekezaji ukiongezeka kutoka dola milioni 200 mpaka zaidi ya dola bilioni 35 hivi sasa.

    "Sasa ni wakati muafaka ushirikiano kuimarika hususan baada ya Rais wa China kuanzisha mpango wa kukuza na kuimarisha ushirikiano na mabara mbalimbali ikiwemo Afrika ambapo mipango na maendeleo kwa pande mbili"anasema.

    Anasema maamuzi au mapendekezo yaliyotolewa yapelekwe kwenye serikali za nchi zote pamoja na baadhi ya mapendekezo kujumuishwa katika Mkutano wa Jukwaa la Fursa za Biashara (FOCAC) kwa ajili ya kutekelezwa na nchi.

    Kauli mbiu ya mkutano huo wa nadharia na mikakati halisi ya vyama vya siasa Afrika–China katika kutafuta maendeleo kwenye nchi itasaidia vyama katika kukuza ushirikiano, kubadilishana mawazo na kutoa uzoefu jinsi ya kushiriki katika amendeleo.

    Mkuu wa idara ya mahusiano ya kimataifa na Waziri wa Mahusiano ya Kimataifa ya CPC, Song Tao anasema China ipo tayari kutoa ufadhili wa makada zaidi ya 4,000 katika ushirikiano na ujenzi wa Vyama pamoja na usimamizi wa serikali.

    Anasema vyama hivyo vinakutana kuangalia njia bora za ushirikiano katika kusfikia mafanikio kwa kutumia mazingira ya nchi husika kwa kuona makundi yote ya kijamii kushiriki katika manufaa ya nchi.

    "Ipo haja ya kuheshimu haki ya binadamu na kujenga jamii iliyo bora kwa afrika kutumia njia bora kujiletea maendeleo kwa kutumia mpango wa maendeleo Afrika"anasema.

    Anataka CPC na vyama vya Afrika kuwa kichocheo cha maendeleo kwa kutumia sera za ndani na nje katika kujenga uwajibikaji na ushirikiano kwa China na Afrika.

    Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd anavishauri vyama vya ukombozi barani Afrika kuwa kama vinataka kuendelea kukaa madarakani ni lazima kuweka mikakati ya kutetea maslahi ya wanyonge na kupiga vita rushwa kwa kuhimiza utendaji kazi kwa maslahi ya wengi.

    Anasema kuja kwa vyama ambavyo si vya ukombozi barani Afrika kumeonesha kuwa vyama vya kisiasa vilivyoleta uhuru vinapigwa vita na mabepari na mabeberu duniani kwa lengo la kuviondoa madarakani vyama vilivyoleta uhuru Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako