• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Historia, asili ya Wachina katika Makumbusho

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:37:16

    Na Oswero

    Makumbusho ni jengo au taasisi penye maonyesho ya vitu vya kale, kazi za sanaa, sampuli za malighafi au vifaa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya jamii.

    Mkusanyiko wa aina hii hulenga kuonyesha mifano ya sanaa, utamaduni, teknolojia au mazingira asilia kwa manufaa ya kuwaelimisha watazamaji.

    Kuna makumbusho ya aina mbalimbali yanayokazia fani fulani za elimu kama vile makumbusho ya historia, ya sanaa, ya teknolojia ya sayansi na kadhalika.

    China ni moja ya nchi duniani zinazothamini na kuenzi utamaduni wake pamoja na kutunza historia katika makumbusho mbalimbali.

    Kuna makumbusho ya taifa lakini pia yapo makumbusho binafsi yanayomilikiwa na watu binafsi, lakini kimsingi yote yanalenga kuweka kumbukumbu ya historia na utamaduni wa nchi.

    Takwimu zinaonyesha kuwa kuna makumbusho binafsi yapatayo 2,000 nchini China, asilimia kubwa yakiwa yakiwa jijini Beijing na mengine yako katika majimbo mengine nje ya Beijing, ambayo ndo mji mkuu wa nchi hiyo.

    Wilayani Chaoyang, katika mji wa Jinzhan, nje kidogo ya jiji, kuna Makumbusho maarufu ya Guanfu iliyo chini ya umiliki binafsi. Makumbusho haya yalianza rasmi mwaka 1997, mwanzilishi wake akiwa Bw. Wa Weidu.

    Ni eneo maarufu na mashuhuri ambapo vitu mbalimbali vya kale vimehifadhiwa kulinda, kutunza na kuelezea historia, asili na jamii ya Wachina.

    Baadhi ya vitu vinavyopatikana kwenye makumbusho haya ni pamoja na vyungu vya kale vya dhahabu, samani mbalimbali, kazi za sanaa za jamii ya wabudha pamoja zana mbalimbali za kale zilizotengenezwa kwa teknolojia ya zamani.

    Jengo hilo limegawanyika katika sehemu mbalimbali ikiwemo vyumba maalum kwa ajili ya maonyesho ya ufinyanzi, samani za kale, upakaji rangi na mengineyo na ndani yake pia kuna duka maalum kwa ajili ya kununua vitu mbalimbali vya nyumbani, nguo, vitabu na vifaaa vya ofisini.

    Bw. Wa, mwanzilishi wa makumbusho haya, anasema kwa sasa wanapokea jumla ya watalii zaid ya milioni moja kwa mwaka, wengi wao wakitoka ndani ya China na baadhi wakiwa ni kutoka nje ya nchi.

    "Makumbusho haya yamekuwa ni daraja muhimu yanayochochea na kuhuisha mawasiliano kati ya jamii na tamaduni za zamani na mfumo wa maisha ya sasa na jamii ya Wachina na namna yao ya maisha, historia, asili na tabia," anasema Bw. Wa.

    Zaidi ya kuwa na makao makuu yake jijini Beijing, mwanzilishi wa makumbusho haya anasema kuwa hadi sasa wameshafungua matawi mengine mawili katika miji ya Shanghai na Xiamen, ambayo pia yanatembelewa na watu wengi sana.

    Hadi sasa, anasema kuwa watu wanaotembelea majengo hayo muhimu kwa ajili ya makumbusho imekuwa kubwa zaidi na ndani ya miaka mitatu wanategemea kufungua jengo lingine jijini Beijing, ili kuweza kuwahudumia wageni kwa ufasaha na ufanisi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako