• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jina la barabara ya urafiki kati ya China na Afrika latokana na hadithi moja ya kusisimua

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:39:05

    Zhang Xiaokun

    Barabara ya urafiki kati ya China na Afrika ni barabara moja iliyoko kwenye mji wa Nyala, jimbo la Darfur, nchini Sudan. Barabara hiyo ni muhimu sana kwa watu wanaoishi kwenye sehemu hiyo, ina athari kubwa kwa maendeleo ya uchumi, mawasiliano ya biashara na maisha ya watu wa eneo hilo. Mwaka 2015, barabara hiyo ilipewa jina la barabara ya urafiki kati ya China na Afrika na wenyeji wa eneo hilo na askari wa uhandisi wa kikosi cha kulinda amani cha China barani Afrika. Jina hilo linatokana na hadithi moja ya kusisimua, na mimi ndio mtu niliyeshuhudia hadithi hiyo.

    Mwaka 2015 mwezi Novemba, mimi nilikuwa dereva wa gari la upakuaji. Siku moja alasiri, tuliamriwa kufanya uhandisi wa kutandaza barabara, ambapo jukumu langu lilikuwa kuendesha gari la upakuaji kusawazisha udongo unaoletwa na kuwekwa kwenye sehemu ya mbele, na kifaa cha kusawazisha ardhi na kukandamiza zinafuata gari langu na kufanya kazi kwa mstari moja. Muda wa kumaliza kazi ulikaribia kufika, na mbele bado kuna kipande cha kama mita ishirini hakijatandazwa, kama hatutasimamisha vitendea kazi, hakika tutamaliza kutandika barabara iliyobaki kabla ya muda kufika.

    Wakati huo huo, wanaume wanne au watano waliruka kutoka kati ya watu waliosimama kando ya barabara, na kuzuia kithabiti gari langu, na kusema haraka kitu fulani kwa lugha ya kienyeji. Baadaye, watu wote waliokuwa kando walikuja kuzingira gari langu, na kuelekeza gari langu, kama wananitaka niangalie kitu fulani. Mara moja nilishtuka na kutokwa jasho sana, nikifikiri kuwa gari langu limekanyaga mtu. Nilitumia kifaa cha mawasiliano ya ndani kuripoti kwa kituo cha kamanda, huku nikiangalia vitendo vya watu wanaozingira gari langu.

    Taratibu nikaelewa kuwa watu hao hawana nia mbaya, nikashuka kwenye gari langu na kukagua, nikagundua gari langu linatoa moshi mweupe, kumbe mpira wa kuingiza maji kwenye chombo cha kuhifadhi maji umekatika. Maji yaliyohifadhiwa yanakaribia kwisha. Ingawa tukio la gari kukanyaga watu halitokei, tatizo hilo la gari bado ni suala muhimu katika jukumu la kulinda amani. Kama vifaa vitaendelea kufanya kazi, injini itaharibika na hata kutofanya kazi tena kutokana na vifaa kupata moto kupita kiasi, hivyo kusababisha msafara kushindwa kurudi leo usiku. Hivi karibuni, jeshi la serikali ya Sudan na upande wa upinzani vimeendelea kupambana, usalama wa jamii umezidi kuwa mbaya, mgogoro wa kikabila unapamba moto zaidi, na kusababisha vifo na majeruhi ya watu mia kadhaa, na matukio mengi ya uporaji. Kwa kawaida matukio hayo yanatokea usiku, hivyo kama hatutaweza kurudi kwa wakati, tutakabiliwa na hatari nyingi.

    Fundi anayeongozana na msafara wetu alikuja kuchunguza gari. Kwa kuwa hakuleta vifaa husika, anapaswa kutumia plastiki, waya wa chuma, gundi ya karatasi na vifaa vingine kurekebisha kidogo mpira. Lakini tatizo la kuvuja maji bado halijatatuliwa. Kituo cha kamanda kinatoa amri ya kurudi, wenzangu wote wanamimina maji yao ya kunywa kwenye chombo cha kuhifadhi maji, lakini maji hayo ni kidogo, gari halitafika mbali maji yote yatavuja. Kama tukitaka kufanikiwa kambini, ni sharti kuhakikisha tuna maji ya kutosha. Ni njia pekee kuendesha gari huku tukiendelea kutia maji.

    Sehemu hiyo tuliyopo ni umbali wa kilomita ishirini kutoka sehemu ya karibu kabisa ya kupata maji, na barabara ni mbaya, kama wakati huo tukienda kuchukua maji, itakuwa usiku tutakaporudi, na hatuwezi kuhakikisha usalama wetu. Mwezi Desemba ni majira ya joto nchini Sudan, maji yana thamani kama mafuta, wenyeji wanachukulia maji kama hazina. Ni jambo la kawaida kuona raia wanakunywa maji machafu moja kwa moja kando ya barabara baada ya kunyesha mvua. Kuwaomba maji ni jambo ambalo haliwezi kufanikiwa.

    Baada ya kufahamu hali hiyo, mwanaume mmoja anamwambia ofisa wa kikundi cha utafsiri anaweza kutatua suala hilo, baadaye, aliondoka akikimbia. Mara moja, matumaini yetu yakawa kwake, tulitumai aliyosema ni kweli. Baada ya dakika kumi, mwanamume huyo alikuja ukweli akichukua pipa moja, ambalo lilimchosha na kumfanya atoke jasho sana. Alitupatia pipa hilo lililojaa maji, karibu lita thelathini. Baada ya kuona maji, wenzetu kama taa inayokaribia kwisha mafuta, inatiliwa mafuta na kuwaka ghafla, wote wanamshukuru mwanaume huyo.

    Lakini, kutokana na gari lilivyoharibika na umbali kutoka hapa hadi kambini, fundi anakadiria bado tunahitaji maji lita 200, maji yaliyoletwa na yule mwanaume hayatoshi. Wakati huo huo, raia wanaoangalia kando kando wanaanza kujadiliana, yule mwanamume anakwenda karibu na raia na kusema kitu kwa sauti chini, baadaye anatuambia kwa furaha, anasema raia wanaweza kukusanya maji lita 200 kwa ajili yetu. Hatuna maneno ya kueleza shukrani zetu, wenzangu wanasema mara kwa mara sentensi moja ya kiingereza "Thank you".

    Baada ya dakika ishirini, raia wanakuja wakichukua ndoo na beseni, huyu analeta maji lita hamsini, yule analeta maji lita thelathini, mwingine analeta maji lita kumi. Askari wetu wanapokea maji hayo, kwa jumla ni lita 200. Maji hayo mengi ni ya kunywa raia, pia ni maji machafu. Wenzangu walipoona sura za raia zikiwa na kicheko cha dhati, na kuona wanamimina maji kwa makini, machozi yalibubujika kutoka machoni mwao. Mimi pia nilisisimka, shukrani moyoni mwangi ilikuwa kama mkondo wa joto unatiririka kutoka moyoni hadi tumbo, tena kutoka tumbo hadi moyoni.

    Baada ya kumaliza kutandika barabara hiyo, barabara hiyo ilipewa jina la barabara ya urafiki kati ya China na Afrika na wenyeji na askari wa uhandisi wa kikosi cha kulinda amani cha China. Kutokana na kukumbusha jina hilo, serikali ya sehemu hiyo inajenga mnara moja, na mkuu wa jimbo la Darfur Bw. Adam El Faki anaendesha sherehe ya uzinduzi. Kuanzia hapo, barabara hiyo kweli imekuwa barabara ya urafiki kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako