• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uzoefu wangu barani Afrika-Zhang Yong

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:39:47

    Nilihitimu masomo ya chuo kikuu mwezi wa Julai, mwaka 2012, nikiwa na umri wa miaka 24, na kuajiriwa na kampuni ya kimataifa ya ushirikiano wa teknolojia na uchumi ya Liaoning. Mwishoni mwa mwezi wa Agosti, nilitumwa barani Afrika kutekeleza mradi wa msaada wa teknolojia ya kilimo wa kampuni yangu. Nilifurahi kupata habari hiyo, lakini pia nilikuwa na wasiwasi. Nilijua kuwa hii ni fursa nzuri na pia ni changamoto kubwa. Mpaka sasa nimefanya kazi barani Afrika kwa miaka mitano, na nina mengi ya kukumbuka..

    Mwaka ule nilitumwa kwenda katika kijiji cha Gegedu, jimboni Divo, Côte d'Ivoire. Joto lilikuwa linafikia hadi nyuzi 40 kwa wastani kwa mwaka. Hali ya usalama, afya na maisha si nzuri.

    Nilipokuwa chuo kikuu nilisomea mambo ya kilimo. Hivyo kazi yangu ni kuzalisha mbegu za mpunga unaohimili mazingira magumu, kutengeneza vitalu vya mbegu za mpunga na kutoa mafunzo kwa wakulima wa hapa. Chakula kikuu kwa watu wa huko ni muhogo na ndizi. Kutokana na ukosefu wa uzoefu wa kulima mpunga, mchele ni chakula chenye bei ya juu kwa familia za kawaida. Hali ya hewa ya Cote d'Ivoire ni ya mvua ya misitu ya kitropiki ambayo inafaa kwa kilimo cha mpunga mara mbili hadi tatu kwa mwaka. Hali hiyo ya hewa inarahisisha mchakato wa kuzalisha mbegu mpya za mpunga unaohimili mazingira ya hapa. Katika mwaka wa kwanza nilipoanza kazi y, niliwajibika eneo la majaribio lenye hekta 5 na kuwaongoza wakulima 6. Kutokana na kazi nzuri yangu, katika mwaka wa pili, nilisimamia eneo la majaribio lenye hekta 10.4 na wakulima 10. Kuanzia mwaka wa tatu mpaka sasa, nilianza kutoa mafunzo kwa wakulima wa hapa.

    Ndani ya miaka hizo mitano, nilizalisha mbegu mpya aina zaidi ya 10 zenye ubora mzuri zaidi kuliko mbegu wa zamani wa hapa na kutumiwa kwa wengi nchini humo na kusifiwa na serikali na watu wa Cote d'Ivoire.

    Licha ya kazi, pia nimepata marafiki wengi. Ingawa niliwahi kuporwa kwa banduki kwa mara mbili, kuathiriwa na mapambano mawili ya kijeshi nchini humo na kupata malaria, lakini niliipenda nchi hiyo ya Afrika. Katika mambo mengi niliyokumbwa nayo, ni mambo matatu ninayokumbuka zaidi.

    Jambo la kwanza

    Mwaka 2013, mwezi wa Juni, niliendesha gari kwenda kazi. Siku hiyo mvua ilikuwa inanyesha, nilipokuwa nalipisha gari lililogongwa, gari langu lilinasa kwenye matope. Nilijaribu kuwapigia simu wenzangu, simu yangu ilipoteza mtandao. Wakati ule, sikujua la kufanya. Baada ya dakika 10, vijana kadhaa waliovaa nguo safi walikuwa wanapita. Hata bila kutegemea, walinisaidia kusukuma gari langu hadi barabarani. Nguo zao safi zilichafuka. Lakini hawakulalamika hata kidogo. Nilitaka kuwapa fedha kuwashukuru. Lakini, walikataa na kusema, wananishukuru sana kuwawezesha kula wali kila siku. Kabla ya kuja kwa wataalam wa China, walikuwa wanakula muhogo tu.

    Jambo la pili

    Mwaka 2017, mwezi wa Septemba, nilisafiri kwenda mji wa Ganio, umbali wa kilomita 200 kutoka nilipofanya kazi. Kwa bahati mbaya, matairi ya gari yangu yaliharibika njiani. Tuliokumbwa na tatizo hilo kutojua kufanya, vijana wawili walikuja na kutuuliza na kutusaidia kubadilisha matairi kutoka kwenye gari na kutupeleka hadi mji pamoja na matairi ili kuyarekebisha. Halafu waliturudisha kwa gari na kutusaidia kuweka matairi kwenye gari na kutusindikiza hadi tulipotaka kwenda. Walisema, walikuwa na umri wa miaka 19 na 22. Kila mwaka, wanakijiji wenzao walikuja kushiriki kwenye mafunzo yangu. Hivi sasa, wanaweza kula wali kila siku na maisha yao yameboreshwa. Walisema, huo ndio msaada wa wachina, wachina wote ni marafiki wa dhati. Wataalam wote waliofanya kazi katika kijiji cha Gegedu watapata msaada wakati wowote nchini humo.

    Jambo la tatu

    Mwaka 2016 na mwaka 2017 tulitoa mafunzo mara mbili kwa wakulima 80 wa Cote d'Ivoire, kuwafahamisha matokeo yaliyopatikana katika utafiti wetu na kuwajulisha uzoefu wa kupanda mpunga. Mafunzo hayo yalisifiwa na idara ya biashara ya ubalozi ya Cote d'Ivoire. Hata mpaka sasa, wanafunzi wetu wanatushukuru na kuripoti hali ya mazao yao na mafanikio yaliyopatikana nao katika kuongeza mavuno.

    Kazi hiyo barani Afrika imenifundisha kuwa ni bora kwa mtu mmoja kuwasaidia zaidi wengine. Pia nimejua umuhimu wa msaada wa China kwa bara la Afrika. Watu wa rangi tofauti wanashirikiana chini ya pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na kuleta maslahi ya pamoja. Nina imani kuwa, kutokana na jitihada za watu wa China na wa Afrika, maisha ya waafrika yataendelea kuwa mazuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako