• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanga wa jua wa China unaokuwepo kwenye msitu wa kahawa wa Ethiopia---Hadithi yangu niliyokuwepo Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-06 09:40:18

    Jina langu ni Li Lin, niliwahi kufanya kazi katika kampuni moja ya China mwaka 2013. Katika mwaka ule, nilipata fursa ya kwanza ya kuitembelea Ethiopia, nchi yenye utajiri mkubwa wa maliasili, na mustakbali mzuri wa maendeleo ya uchumi. Nilifurahia sana safari yangu hiyo barani Afrika, licha ya kutembelea Ethiopia, pia nilitaka kutafuta fursa za biashara kwenye sekta ya kilimo.

    Mwanzoni mwa miaka yangu miwili nchini Ethiopia, nilizihudumia idara za kilimo za Ethiopia kwa kuzipatia huduma ya teknolojia, pia nilipata nafasi ya kufahamiana na rafiki yangu mkubwa Bw. Abiyot, ambaye amekuwa mshirika wangu mkubwa wa biashara.

    Bw. Abiyot ni mwenyeji wa kabila la Oromia, ambaye baba yake ni mfanyabiashara wa kahawa. Kwa hiyo, alinifahamisha ujuzi wa kahawa ya kiwango cha juu duniani mara kwa mara, huku akitaka niwajulishe Wachina wengi zaidi. Tulianza kushirikiana na kuanzisha kampuni yetu ya kuuza kahawa nje ya Ethiopia, ili kutoa nafasi ya kuwauzia wafanyabiashara kahawa moja kwa moja, na kampuni yetu imekuwa kampuni ya kufanya biashara kati ya China na Ethiopia.

    Nilianza kutembelea mashamba ya kahawa pamoja na wenzangu wa Afrika, na kufanikiwa kujifunza mambo mengi. Kisha nikarudi China na punje za kahawa nilizochagua kwa makini katika bustani hizo za Afrika.

    Ingawa umri wangu ni zaidi ya miaka 40, nililazimika kurudi tena darasani, kupata masomo ya kitaalamu ya utengenezaji wa kahawa.

    Walimu wangu wamesema Ethiopia ikiwa ni chimbuko la kahawa duniani inawavutia watu wengi. Lakini soko la kahawa ya Ethiopia limedhibitiwa na nchi za Ulaya, Marekani, Japan na Korea Kusini. China haina budi kuchagua kahawa iliyobaki, au kununua kahawa hiyo kutoka Japan na Korea Kusini kwa bei kubwa. Kwa hiyo, nina imani kubwa ya kuiletea China moja kwa moja kahawa ya Ethiopia yenye sifa nzuri.

    Baada ya mafunzo, nilirudi tena katika eneo la milima la uwanda wa juu nchini Ethiopia, ambako kilomita 500 kutoka mij mkuu Addis Ababa, na kulazimika kuendesha gari kwa zaidi saa ya 13. Tulipita barabara kuu ya kipekee nchini Ethiopia, ambayo ilijengwa na China. Njiani tuliweza kuona mandhari ya kupendeza ya mto, pia tuliweza kuona makundi ya ngamia wanaokunywa maji kando ya mto. Baada ya kupita barabara kuu, tulianza safari yetu katika njia zilizoko mlimani, ambazo ni vigumu kwetu kutembea. Hatukuwa na budi kuendesha pikipiki kwa kasi ndogo, hasa ilituchukua muda wa saa nzima kwa umbali wa kilomita 20 tu. Wenyeji wanapenda kujenga makazi nyumba zao milimani. Wanapanda kahawa mlimani na kukabiliana na mahitaji ya maisha yao.

    Wenyeji ni wakarimu na watu wenye tabasamu. Mimi nilikuwa mgeni wa kwanza kwao kumuona. Mwanzoni, waliniangalia kimya kimya, watoto wachache tu wakanifuata ili kuangalia nafanya nini. Mtoto Nati mwenye umri wa miaka minane, ni mmoja wa watoto wa mama mpishi katika kiwanda chetu cha kutengenezea kahawa. Nati alifurahi kukutana nami, pia amekuwa mwalimu wangu wa lugha ya kienyeji. Aliambatana nami kila mara, na alinisaidia sana katika maisha na kazi zangu.

    Niliishi na kufanya kazi pamoja na wenyeji kila siku, tulichuma kahawa pamoja, tuliyachagua na kuikausha kwa pamoja. Baadhi ya wakati, nilichukua vifaa maalumu wasivyofahamu ili kupima kiasi cha sukari, uzito, na maji ndani ya kahawa, pia niliwahi kutumia chombo cha GPS na kuandika mahali tuliopo na mwinuko wake, pamoja na hali ya ukuaji wa kahawa. Baada ya siku nyingi, wenyeji walianza kunipenda kutokana na jitihada zangu. Nilipenda kusikiliza nyimbo walizoimba, ambazo zinabeba matumaini yao kwa maisha mazuri.

    Msimu wa mavuno ni kipindi chenye furaha pamoja na uchovu, ambao mapato yote katika mwaka mzima yanapatikana katika muda huo. Akina mama na watoto wanachuma kahawa mlimani, na wanaume wanafanya kazi ya kusafirisha hadi kwenye viwanda vya kukoboa kahawa. Watoto wadogo hutembea kwa miguu kwa saa zaidi ya moja, ili kutuletea mifuko ya kahawa yenye uzito wa kilo moja na kutuuziakwa nusu dola. Wanatumia pesa hizo kununua vifaa vya shule au chumvi. Kwa watoto hao, miezi miwili hivi ndiyo kipindi cha kuchuma pesa kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji ya maisha yao, au kununua vitu wanavyopenda mjini. Niliwahi kumwona mjamzito aliyebeba mzigo wa kahawa ya kilo 10, ili kuchuma pesa kwa ajili ya kumpatia mtoto wake wa nne atakayezaliwa maisha bora zaidi. Machoni mwa wakulima hao wa Ethiopia, kahawa ni sehemu kuu ya mapato katika maisha yao, pia ni matumaini yao kwa maisha bora zaidi. Ingawa siyo kazi rahisi, lakini wanaridhika na maisha ya hivi sasa.

    Mwaka 2017, nilikwenda tena Ethiopia pamoja na walimu wangu wa China wa kutengeneza kahawa, wateja wangu wakuu, na mabingwa katika mchuano wa utaalamu wa kutengenezea kahawa China, ambao wanapenda kahawa ninayotengeneza pamoja na wenzangu wa Ethiopia. Walitaka kuitembelea sehemu hiyo, na kushiriki kazi ya mavuno. Aina hiyo ya biashara ya kahawa ni ya moja kwa moja, yaani "kutoka kupanda miche hadi kunywa". Wateja wa China wanakuja kwenye chimbuko la kahawa, na kuiletea China moja kwa moja baada ya mchakato wa kuchagua, kukoboa, kukausha, kuondoa maganda na kuchagua tena kwa mikono huko Ethiopia, hatimaye kahawa yenye ubora zaidi inafikishwa China. Mambo hayo yote yamewafahamisha wenzangu wa Ethiopia kwamba jitihada zao zina maana kubwa, wamejionea fahari kutokana na kutengeneza kahawa yenye ubora na kujenga daraja kati ya wakulima wa kahawa wa Ethiopia na wafanyabiashara na wateja wa China.

    Mwanzoni niliwahi kuona kuwa nitailetea sehemu hiyo ya Ethiopia mabadiliko makubwa. Lakini baada ya muda mrefu, nimeona kuwa aliyepata mabadiliko makubwa ni mimi mwenyewe. Wachapakazi na watoto wa kupendeza wa Ethiopia wamenipatia msaada mkubwa nilipokuwa nje ya nchi yangu. Nimepata mengi ya kujifunza kutoka kwao, ambao wanapenda maisha na kuwaamini watu kwa kutumia moyo safi. Kwangu kahawa siyo tu ni aina ya kinywaji, bali pia imekuwa sehemu muhimu katika maisha yangu. Ethiopia sasa pamekuwa ni nyumbani kwangu pengine ninapopapenda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako