• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ushirikiano China na Tanzania waongezeka mara kumi kwa miaka sita na kufikia Trilioni 15.82

    (GMT+08:00) 2018-08-14 09:28:47

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR- ES-SALAAM

    USHIRIKIANO wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali unimarisha kila mwaka katika kuhakikisha nchi hizo mbili kila moja inanufaika .

    Ongezeko hilo limefanya uwekezaji wa China nchini Tanzania kuongezeka mara kumi katika kipindi cha miaka sita kutoka Sh trilioni 1.58 hadi kufikia Sh trilioni 15.82.

    Hayo yalibainika hivi karibuni wakati Rais John Magufuli alipofanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Wang Ke ambaye pia aliwasilisha barua kutoka kwa Rais wa China.

    Katika mazungumzo hayo Balozi Wang anamueleza Rais Magufuli kuwa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na China umeendelea kukua kwa kasi kubwa hususani katika masuala ya kiuchumi.

    Anasema miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa, na katika kipindi cha miaka sita iliyopita uwekezaji wa China nchini Tanzania umekuwa mara kumi kutoka Sh trilioni 1.58 hadi kufikia Sh trilioni 15.82.

    Balozi Wang alimhakikishia Rais Magufuli kuwa China itaendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya Tanzania.

    Kuhusu ombi alilolitoa Rais Magufuli wakati meli ya matibabu ya China ilipokuja nchini Novemba mwaka jana, Balozi Wang Ke alisema Rais wa China ameshafanyia kazi ombi hilo kwa kutoa udhamini wa masomo kwa Madaktari 20 watakaosomea ngazi ya Uzamili na Uzamivu katika matibabu ya ini na uboho (bone marrow) katika Chuo Kikuu cha Shandong cha China, na pia nafasi 30 za wataalamu watakaohudhuria semina ya mafunzo ya usimamizi wa hospitali.

    Rais Magufuli anamshukuru Rais Xi kwa kutoa nafasi hizo za masomo na kwa mchango mkubwa wa China katika maendeleo ya Tanzania, na alimuomba Wang Ke kufikisha ujumbe wake kwa Rais Xi kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa kidugu na kihistoria na China.

    Rais Magufuli anatoa wito kwa Wang Ke kuendelea kuwahimiza wawekezaji zaidi kuja kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili na kwamba Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.

    Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezechiel Nibigira ambaye amewasilisha barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza.

    Aidha, Rais Magufuli alifanya mazungumzo na Nibigira, mazungumzo ambayo yalihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Susan Kolimba na Balozi wa Burundi nchini Gervais Abayeho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako