• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • JUHUDI ZA KUONDOA UMASKINI AFRIKA KUPITIA USHIRIKIANO

    (GMT+08:00) 2018-08-16 09:13:30

    Na Trix Ingado

    Kati ya malengo ya ushirikiano endelevu kati ya Africa na China kuondoa janga la umaskini ni mojawapo ya malengo kuu. Licha ya dharura iliyoko katika kuondoa umaskini barani Afrika , ni muhimu kuzingatia kwamba sio jambo rahisi kukabiliana nalo.

    Malengo ya umoja wa mataifa ya mwaka wa 2030 yanatilia mkazo kumaliza umaskini, kubadilisha maisha ya waathiriwa na kulinda mazingira kote duniani.

    Ushirikiano kati ya china na afrika utasaidia pakubwa katika juhudi hii, kama tunavyojua, mwakani 2015 China ilitoa dola elfu sitini za uwekezaji Afrika. Bilioni tano zilitolewa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo wa china na afrika. Hii ni ishara ya kwamba pande hizi mbili zinadhana sawia kuhusu vita dhidi ya umaskini.

    Mnamo tarehe kumi na tano mwezi wa nane ofisi kuu ya kuondoa umaskini ya baraza kuu la taifa liliandaa kongamano kuu lilihudhuriwa na maafisa wa serikali, wafanyabiashara, na wasomi zaidi ya mia tatu .

    Wageni hawa kutoka marekani, Japan, Denmark na nchi arobaini za bara Afrika walijumuika kuzungumza kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika chini ya mpango wa Njia Moja Ukanda Mmoja.

    Katika matamshi yake mkutanoni waziri LIU Yongfu alisema kwamba, kazi inayotekelezwa katika mpango wa Njia Moja Ukanda Mmoja ni muhimu katika ujenzi wa miundo mbinu zitakazo fanikisha malengo ya umoja wa mataifa ya mwaka 2063.

    Wosia wake uliungwa mkono na Bi. Sacko aliyesema kwamba ushirikiano kati ya muungano wa Afrika na China katika kuendeleza sekta za ukulima, technolojia, ukulima na ufugaji wa mifugo na samaki umewaelimisha wengi barani Afrika. Hii ni kupitia wataalamu wa Kichina waliotangamana na wenzao Waafrika.

    Wajumbe hao wanatarajiwa kuzuru mji wa Bije, mkoani Guizhou kati ya tarehe kumi na tano na kumi na sita mwezi wa Agosti. Ziara hii itawapa fursa ya kujionea miradi ya kupunguza umaskini kupitia ujenzi wa miundo mbinu, ujenzi wa viwanda, udumishaji wa mazingira, utalii na kadhalika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako