• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanadiplomasia wanasema FOCAC unaashiria mwamko mpya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-08-24 09:52:11

    Na Eric Biegon – NAIROBI

    Wanadiplomasia wameelezea matumaini yao kuwa ushirikiano kati ya Afrika na China kupitia Jukwaa la Forum on China-Africa Cooperation (FOCAC) utaleta enzi mpya ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

    Wanadiplomasia kutoka pande zote mbili wanaamini kuwa FOCAC ni jukwaa ambalo litachochea ukuaji wa nchi za bara Afrika, hasa kutokana na hatua zilizopigwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.

    Mabalozi wana maoni kuwa mkutano wa FOCAC uliofanyika mwaka 2015 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, uliinua viwango vya mahusiano kati ya China na Africa kufikia hatua mpya ya historia kufuatia makubaliano mbalimbali yaliyoibuliwa katika mkutano huo

    Ni hapa ambapo Rais wa China, alizungumzia kuimarishwa kwa mausiano hayo na kutangaza FOCAC kama mpango halisi na dhabiti ya kukuza maendeleo kati ya China na Afrika.

    Kiongozi huyo wa China alitangaza mfuko wa fedha wa dola bilioni 60 za Marekani ili kusaidia mipango ambayo ingeashiria mwamko wa Afrika.

    Fedha hizo zililenga maeneo ya viwanda, kilimo, usasa, miundombinu, ufadhili wa miradi, maendeleo ya kijani, uwezeshaji wa biashara na uwekezaji, kutokomeza umaskini na kufanikisha ustawi wa watu, ubadilishanaji wa utamaduni na kutangamana kwa watu kutoka pande zote mbili pamoja na kuimarisha amani na usalama.

    Tathmini ya hatua zilizopigwa hadi sasa, kulingana na Balozi wa China nchini Kenya Sun Baohong zinaonyesha kuwa FOCAC ni mfumo muhimu ambao umetoa faida unaoonekana kwa watu wa Afrika.

    "Katika miaka ijayo, tutaratibu rasilimali za makampuni ya Kichina, vyombo vya habari, taasisi za Confucius, jamii ya wachina iliyoko nje na watalii wa Kichina, na kuendelea kujenga majukwaa ya ushirikiano wa China na Afrika katika Kituo cha Pamoja cha Utafiti pamoja na ile ya utamaduni." alisema

    Katika hotuba yake ya kwanza alipochukua uongozi wa ofisi ya balozi jijini Nairobi mwezi Mei, Sun alibainisha kuwa "FOCAC imeleta matumaini na fursa kwa pande zote mbili." Fursa hizi zinabadilika na kuwa na hali halisi, alisema.

    Sun anasema mkutano ujao wa FOCAC, utakaofanyika Beijing mwezi Septemba ni muhimu, kwani utaleta mchango mkubwa katika maendeleo ya mahusiano ya baadaye ya China na Afrika.

    "Tukio hilo ni muhimu sana. Chini ya hali ya sasa ya kimataifa, viongozi kutoka China na nchi za Afrika watakusanyika Beijing kujadili ushirikiano wa kirafiki, na kujenga jamii ya pamoja ya China na Africa na kuchunguza njia na hatua za kuimarisha ujenzi wa mfumo wa mkanda mmoja njia moja." alisema.

    Maneno yake yanaakisi vizuri na yale ya Balozi Christopher Chika, ambaye ni mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya.

    Kwa maoni yake, FOCAC ni muhimu katika utekelezaji wa uhamisho wa utafiti na teknolojia kutoka taifa hilo la pili kwa ukubwa kwa uchumi wa dunia kuelekea bara la Afrika.

    "Ndoto yetu ni kwamba uchumi wetu utapata msukumo wa kiteknolojia. Hivyo ushirikiano wowote ambao utatusaidia kuboresha ujuzi wetu na kuhamisha teknolojia unakaribishwa sana. Bila shaka lazima tushughulikie hilo, kwani hilo ndilo jambo litakalofanya uchumi wetu kukua kwa kasi na kuzalisha ajira tunazohitaji kwa idadi kubwa ya vijana wetu wasio na kazi. " Alisema.

    Wanadiplomasia hao wawili wanasema mpango huo ni moja ambao unawezesha mazungumzo ya pamoja na ushirikiano halisi kati ya China na Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako