• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kuiwakilisha Tanzania FOCAC huku akiambatana na waandishi wa habari 10

    (GMT+08:00) 2018-08-29 09:51:38

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    MKUTANO wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unafanyika wiki ijayo Beijing China, kuanzia Septemba 3-4 mwaka huu ikiwa ni fursa nyingine kwa nchi za Afrika kupata fursa mbalimbali za ushirikiano baina ya nchi hizo na China.

    China ambayo ni nchi yenye uchumi mkubwa duniani imekuwa na mipango mbalimbali ya kusaidia nchi za afrika kwa lengo la kuhakikisha nchi hizo zinaendelea na kukua kiuchumi kwa kadri ya mipango ya nchi husika.

    Tanzania ni nchi mojawapo yenye ushirikiano katika Nyanja mbalimbali za uchumi,kisiasa,kijamii na kidplomasia na China na ikinufaika na mipango kadhaa ya nchi hiyo katika utoaji misaada na mikopo ya kifedha,miradi ya miundombinu na sekta nyingine kupitia mkakati wa ukanda mmoja njia moja.

    Katika mkutano wa FOCAC, Ujumbe wa Tanzania utaongozwa na waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye imeelezwa ikiwa ni sehemu ya mkutano huo ataandaliwa nafasi kufanya mazungumzo ya kukuza ushirikiano na Rais Xi Jinping.

    Katika mkutano huo unatarajia pamoja na mambo mengine kuboresha mahusiano baina ya Afrika na China hususan Tanzania katika Nyanja tofauti

    Balozi wa China nchini, Wang Ke anasema katika ujumbe wa Tanzania nchini humo utakaoongozwa na Majaliwa atakayeambatana na waandishi wa habari 10 kutoka vyombo vya habari mbalimbali nchini.

    Wakiwa nchini humo, Waziri mkuu atakuwa na shughuli mbalimbali kwa siku 10 ikiwemo mikutano na viongozi mbalimbali kuhusu ushirikiano wao ikiwemo na viongozi wa serikali ya mitaa,Makampuni ya China na kutembelea mji wa Shenzhen katika jimbo la Guangdong ambao umejengwa kisasa na kuwa na maendeleo mbalimbali.

    Bibi Wang anasema wakiwa katika mji huo watafanya mazungumzo na serikali ya mji huo huku akitembelea kampuni ya teknolojia ya Huawei na nyinginezo kuhamasisha uwekezaji baina ya mji huo na Tanzania.

    Anazungumzia FOCAC yenye nchi wanachama 33 ambao wote wamethibitisha kushiriki pamoja na taasisi za kimataifa 27 zitawakilishwa kwenye mkutano huo huku wakitarajia kuwa na mipango ya maendeleo ya pamoja,kujadili muunganiko wa nchi za Afrika kwa kutumia mkakati wa kiuchumi wa njia moja na ukanda mmoja.

    Bibi Wang anasema pia kuboresha uhusiano wa pande hizo mbili kutokana na kuwa na mtazamo sawa katika masuala mengi kwa kuanzisha sera mpya katika amsuala ya miundombinu,biashara ,ulinzi na usalama na mengineyo.

    Anasema mkutano huo utafunguliwa na Rais Xi Jinping baada ya kutanguliwa na mikutano ya maafisa na mawaziri kutoka pande hizo mbili itakayojadili masuala mbalimbali.

    Baada ya ufunguzi kutakuwa na hotuba mbalimbali za viongozi kutoka nchi za Afrika na baada ya kumaliza Rais Xi atakutana na waandishi wa habari akiambatana na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kuelezea majadiliano na makubaliano yaliyofikiwa kwenye mkutano huo.

    Naye,Mkurugenzi wa idara ya habari (MAELEZO)Hassan Abbas anasema mwaliko wa waandishi hao kuripoti FOCAC ni mafanikio ya idara hiyo kumuomba balozi kuhakikisha wanaimarisha diplomasia kwa vyombo vya habari.

    Anawataka waandishi wa habari wanaoenda kuhakikisha wanajulisha umma wa watanzania yatakayojiri katika mkutano huo na ziara ya Waziri Mkuu katika maeneo mbalimbali atakayotembelea na kufanya mikutano.

    FOCAC ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa ni miaka 18 iliyopita, huku mkutano wa mwisho ulifanyika Johannesburg Afrikakusini kwa pande mbili kukubaliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kama ukuzaji wa viwanda, kilimo, fedha, utalii, usafiri wa anga na mengineyo.

    Inaelezwa kuwa China ilitoa dola za marekani bilioni 60 katika mkutano wake wa afrika Kusini, ikiwemo dola bilioni tano kama mikopo nafuu na isiyo na riba.

    Takwimu zinaonesha kuwa Mpaka Machi,mwaka huu asilimia 90 ya dola bilioni 60 iliyotolewa na China kwa Afrika imetolewa na kutawanywa maeneo mbalimbali huku Julai mwaka huu Mfuko wa Maendeleo wa China na Afrika ukiwekeza kwa zaidi ya dola bilioni 4.6 katika miradi 92 katika nchi 36 za Afrika,ikiongozwa na makampuni ya China kuwekeza dola bilioni 23 Afrika.

    Pia China imetoa ufadhili wa mafunzo na mafunzo ya kitaalamu kwa nchi hizo na kusaini mikataba ya makubaliano ya ujenzi wa uchumi na ushirikiano wa kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako