• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Biashara bidhaa za kilimo China-Afrika yafika $6 bilioni

  (GMT+08:00) 2018-08-29 09:52:22

  Oswero, Beijing

  Biashara ya bidhaa za kilimo kati ya China na Afrika imeongezeka na kufikia dola bilioni 6.02 za Kimarekani mwaka 2017, imeelezwa.

  Mkurugenzi Msaidizi wa Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Kilimo ya China, Bi. Ma Hangtao amesema ushirikiano katika biashara ya bidhaa za kilimo umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.

  Akizungumza wa waandishi wa habari kutoka barani Afrika walioko jijini Beijing katika mafunzo maalum, siku chache kabla mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, FOCAC, Bi. Ma alisema sekta ya kilimo ni moja ya sehemu ambayo jukwaa hilo linaipa kipaumbele cha kipekee.

  Alisema hadi kufikia mwaka jana, 2017, China ilikuwa imeshatia saini ya makubaliano kati yake na taasisi mbalimbali za utafiti barani Afrika ukilenga tafiti katika maeneo mbalimbali ya namna bora ya kuongeza tija katika kilimo na kutatua changamoto zinazoikumba sekta hiyo.

  "Haya makubaliano tuliyoingia na nchi za bara la Afrika zinalenga kuboresha tafiti za kilimo ya namna ya kuongeza uzalishaji na pia katika sekta ya teknolojia ambayo ni msingi muhimu wa maendeleo na mapinduzi ya kilimo," alisema.

  Aliongeza kuwa kwa kupitia kwa makubaliano hayo, nchi za bara la Afrika zinakuwa katika nafasi sahihi ya kuboresha sayansi ya kilimo na teknolojia itakayochangia kuongeza uzalishaji na kuongeza kuboresha mnyororo wa thamani wa bidhaa za kilimo.

  Bi. Ma aliongeza pia kuwa kuanzia mwaka 2006, China imefanikiwa kuameandaa jumla ya mafunzo kwa waatalam wa kilimo yapatayo 337 zilizohudhuriwa na wataalam mbalimbali wa sekta ya kilimo kutoka nchi za bara la Afrika.

  Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na China, Bi. Ma alisema kuwa jumla ya wataalamu wapatao 6,260 kutoka nchi zaidi ya 30 walipatiwa mafunzo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo biashara, mipango na menejimenti ya kilimo.

  Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa hadi kufikia mwaka 2016, serikali ya China iliwekeza jumla ya bilioni 1.27 za Kimarekani katika makampuni yapatayo 108 yanayoshughulika na masuala ya kilimo barani Afrika.

  Aliongeza kuwa kilimo bado ni uti wa mgongo wa uchumi na chanzo cha kipato cha wananchi walio wengi, duniani ikiwemo bara la Afrika huku kikichangia asilimia kubwa ya pato la ttaifa, asilimia kubwa ya ya mapato ya nje na kuajiri karibu asilimia kubwa ya nguvu kazi, hivyo hawana budi kuhakikisha kinapewa kipaumbele na msisitizo unaostahili.

  Alisisitiza kuwa bara la Afrika linaweza kuwa mfano dhidi ya mabara mengine mengine duniani endapo litachukua jitihada za makusudi na njia mbalimbali za kuinua kilimo.

  Alisema kuna kila sababu ya kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kutokana na umuhimu walionao ili waweze kupeleka mbele maendeleo ya sekta ya kilimo duniani.

  Alieleza kuwa China na Afrika zitaendeleza ushirikiano wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo, bisharara, uwekezaji, elimu, afya, miundombinu na kuhakikisha ushirikiano huo unakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako