• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afya 50 kutoka Tanzania kupata mafunzo mahsusi China

    (GMT+08:00) 2018-08-29 14:18:50

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    NOVEMBA mwaka jana, Meli ya matibabu kutoka China iliwasili katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania ikiwa na madaktari bingwa na wafanyakazi 381 ambao walitoa huduma ya matibabu bure ndani ya meli hiyo kwa muda wa wiki moja.

    Meli hiyo "Peace Ark" ilifanikiwa kutoa matibabu bure kwa watanzania 6,441 huku Rais John Magufuli alifanya ziara rasmi ya kutembelea meli hiyo na kuridhishwa na vifaa maalum vya matibabu na wataalamu waliokuwa katika meli hiyo.

    Katika barua ya Shukrani kwa Rais wa China, Magufuli alitamani kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya nchini.

    Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke anasema chini ya maelekezo ya Jinping, mwaka huu wizara ya elimu China na ile ya biashara imetoa ufadhili kwa madaktari 20 kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili, (MUHAS) wanaoenda kupata mafunzo ya uzamili na Uzamivu katika Chuo cha Tiba cha Cheeloo katika Chuo Kikuu cha Shangdong.

    wengine wa wataalam wa afya 30 kutoka hospitali za Taifa, rufaa na zile za mikoa wanaoenda nchini humo katika jimbo la Hunan kwa mwezi mmoja kupata mafunzo mbalimbali katika utoaji matibabu Mahsusi.

    Katika hafla maalum ya kuwaaga wanafunzi hao, iliyofanyika katika ubalozi wa China nchini, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako anasema China imeendelea kujikita kusaidia sekta ya afya nchini baada ya kutoa ufadhili Maalum kusaidia sekta hiyo katika magonjwa mahsusi yenye changamoto katika utoaji matibabu.

    Anasema ufadhili huo umejikita katika kupata wataalamu wa upandikizaji wa Chembe za Damu, utibuji ini, utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wa Saratani,utoaji matibabu ya mionzi, mausla ya ufundi mitambo kwneye utoaji matibabu, ugunduzi dawa zasaratani, mfumo wa viungo vya mwili, saratani ya damu kwa watoto na ufamasia katika kuanzisha viwanda vya dawa nchini.

    Baada ya madaktari hayo kupatiwa matibabu watasaidia kupunguza upelekaji wa wagonjwa nje ya nchi na kuimarisha matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili, (MUHAS) iliyopo katika Kampasi ya Mloganzila.

    Balozi wa China Wang Ke anasema katika elimu, China hutoa ufadhili wa zaidi ya watu 100 kila mwaka ikiwemo 20 wanaosoma katika masuala ya Mafuta na gesi katika minajili ya kukuza maendeleo ya viwanda nchini.

    Anasema kuna watanzania zaidi ya 4,000 wanaosoma nchini China na asilimia 80 inatokana na ufadhili wao na wengi wakisoma masuala ya Mawasiliano, Usafirishaji, Fedha, Uhandisi na mengineyo.

    Ke anasema ushirikiano katika masuala ya afya yana historia kubwa kuanzia mwaka 1964 na 1968 China walianza kupeleka madaktari Zanzibar na Tanzania bara na mpaka sasa watu milioni 22 wamepatiwa matibabu kutoka kwa wataalamu wa afya kutoka China.

    Anasema kwa sasa kuna Madaktari 32 wanaotoa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na Hospitali za Pemba huko Zanzibar.

    Naye, Prof. Joyce Ndalichako anashukuru kwa ufadhili huo ambao ni maalum na kuwa wizara yake kwa kushirikiana na wizara ya afya walishirikiana kuwapata Madaktari waliochaguliwa kusoma taaluma hizo mahsusi kutokana na changamoto iliyopo.

    Anasema kuna upungufu mkubwa wa wataalamu katika maeneo hayo wanayoenda kusoma na kuwataka kusoma kwa bidii na baada kumaliza kuwahudumia watanzania.

    Alisema mbali na kutoa ufadhili huo ambao ni tofauti na unaotolew ana nchi hiyo kila mwaka, wanatarajia hivi karibuni kuzindua Maktaba kubwa na pekee katika nchi za Afrika Mashariki iliyopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako