• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hatua kwa hatua China imekuwa kipenzi cha wanafunzi wanaotafuta masomo ya juu kutoka Afrika

  (GMT+08:00) 2018-09-25 09:02:01

  Na Eric Biegon - NAIROBI

  Mwenendo wa hivi karibuni unaonyesha kuwa China imekuwa eneo la kuvutia kwa Waafrika wanaotafuta masomo zaidi. Kufikia mwaka jana, inakadiriwa kuwa asilimia 14 ya wanafunzi wote wa kigeni katika China wanatoka Afrika. Huu ni ukuaji wa haraka mno kwani mwaka 2003 ni asilimia 2 pekee ya wanafunzi kutoka Afrika waliotafuta masomo China.

  Idadi hii ni kubwa kuliko idadi ya wanafunzi wa Afrika nchini Marekani na Uingereza. Kwa sasa, China ni ya pili, nyuma ya Ufaransa ambayo ni mwenyeji wa asilimia kubwa ya wanafunzi kutoka mataifa yanayozungumza lugha ya Kifaransa.

  Idadi kubwa ya wanafunzi hawa ujisajili kwa shahada ya kwanza, shahada ya uzamili na shahada ya udaktari katika Vyuo Vikuu mbalimbali nchini China. Idadi hii inaendelea kuongezeka kila mwaka.

  Kwa kiasi kikubwa, hii pia imefanikishwa na toleo la udhamini wa masomo kwa wanafunzi kutoka mataifa barani Afrika kutoka kwa serikali ya China. Fursa hizi zinaendelea kuongezeka wakati ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka ya hivi karibuni ukiendelea kunawiri.

  Kuanzishwa kwa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) miaka 18 iliyopita, imechochea mafanikio makubwa katika suala hili. Kupitia jukwaa hili, China iliahidi kutoa fursa zaidi za mafunzo kwa wanafunzi na vijana wa Afrika katika China au katika nchi wanamotoka.

  Mwaka 2015, itakumbukwa kwamba wakati wa mkutano wa FOCAC jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Rais wa China Xi Jinping alitangaza ufadhili wa serikali kwa wanafunzi 30,000 wa Afrika kwa kipindi cha miaka 3.

  Hadi kufikia sasa Beijing imetimiza ahadi hii na tayari imeanza mzunguko mwingine wa udhamini wa masomo kwa muda wa miaka mitatu yajayo (2018-2021) kama ilivyotangazwa kwenye kongamano la FOCAC mwaka huu jijini Beijing. Aidha, China imekuwa kipenzi kwa elimu kwa Waafrika kutokana na kwamba gharama yake ni nafuu.

  Ni dhahiri kuwa China haijakuwa tu mshirika mkuu wa biashara kwa Afrika, lakini pia imekuwa mwekezaji na mwanakandarasi mkubwa barani kwa miaka nyingi. Hakika, mamia ya makampuni ya Kichina yaliyoko Afrika yanatoa maelfu ya nafasi za kazi kwa watu wake.

  Kwa Kenya na eneo la Afrika Mashariki, ushirikiano kati ya pande zote mbili umezaa matunda mema. Ushirikiano kati ya watu kutoka pande hizi nao unaendelea kunawiri.

  Balozi wa China nchini Kenya Sun Baohong hivi karibuni alifichua kwamba katika miaka mitatu yaliyopita pekee, China imetoa zaidi ya fursa elfu 67 ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Kenya kutoka sekta tofauti.

  "Tangu mwaka 1982, serikali ya China imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi wa Kenya kila mwaka. Mimi najivunia sana kuwa China imekuwa moja ya nchi inayopendwa zaidi na wanafunzi wa Kenya." Alisema.

  Hadi sasa, taarifa katika Wizara ya Elimu nchini zinaonyesha kuwa zaidi ya wanafunzi 1,000 wa Kenya wamepata na kunufaika na udhamini wa masomo kutoka Serikali ya China. Chini ya mpango huu, zaidi ya wanafunzi 2,400 wa Kenya kwa sasa wanasoma nchini China.

  Mwaka huu, wanafunzi 69 wa Kenya wamepokea udhamini wa masomo kutoka serikali ya China. Hata hivyo, takriban wanafunzi wengine 100 kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki wamefaidika kupitia udhamini wa masomo kutoka vyanzo vingine nchini China.

  Makampuni makubwa ya ujenzi ya Kichina kama vile China Road na Bridges Corporation (CRBC), kwa mfano, inatoa ufadhili wa masomo kamili kwa wanafunzi bora kujiunga na masomo mbali mbali ya uhandisi.

  "Mtajiunga na miji mbalimbali na vyuo vikuu nchini China kutofuta shahada mbalimbali. Wanafunzi wengi kutoka Kenya ambao walihitimu kutoka vyuo vikuu vya Kichina wamekuwa wakifanya vyema sana katika kazi zao na kuwa uti wa mgongo wa maendeleo wa nchi. "Bi Sun alisema haya alipozindua kundi la wanafunzi ambao walifanikiwa kupata udhamini wa masomo kutoka serikali ya China ya mwaka 2018.

  "Nina furaha sana kuona vijana wengi walio na shauku na imani kwa uwezo wao. Ninyi ni nguvu ya ukuaji, nguvu ya maendeleo na nguvu ya ufunguzi. Munawakilisha matumaini ya Kenya na siku za baadaye ya urafiki katika ya China na Kenya." Aliongeza balozi Sun.

  Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003, mpango wa udhamini wa masomo kutoka serikali ya China imewasaidia mamia ya wanafunzi kutimiza ndoto yao ya kupata masomo zaidi katika China.

  Na huku nchi hizo mbili zinapoadhimisha miaka 55 tangu kuzindua mahusiano ya kidiplomasia, Sun anatumahi kuwa uhusiano kati ya China-Kenya utapata mwanzo mpya utakaoleta ufanisi zaidi.

  "Naamini kuwa, kupitia jitihada za pamoja za pande zote mbili, tutaendelea kupata fursa zaidi za ushirikiano kati ya China na Kenya zitakazozaa matunda mema zaidi." Alisema.

  Kwa upande mwingine, hadi sasa China imeanzisha Taasisi nne za Confucius nchini Kenya. Kituo cha Lugha na Utamaduni iliyoko Chuo Kikuu cha Kenyatta uliofadhiliwa na serikali ya China sasa umekamilika.

  Kituo cha pamoja cha Utafiti kati ya China na Africa kimekuwa jukwaa muhimu kwa ushirikiano wa kisayansi na kiteknolojia pamoja na kuwa kituo cha kukuza vipaji kwa vijana wa Kenya.

  "Idadi ya wanafunzi wa chuo kutoka China wanaotembelea Kenya kwa mazoezi ya kielimu na kijamii inaongezeka. Mwaka jana, idadi ya watalii wa Kichina waliozuru Kenya ilifikia elfu 69 na bado idadi hii inaongezeka. " Sun alisema.

  Bila shaka China itabaki kuwa mshirika mkuu wa Afrika kwa suala la elimu ya vijana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako