• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazao 10 kutoka Tanzania yapata soko China

    (GMT+08:00) 2018-10-16 12:22:44

    Na Theopista Nsanzugwanko,DAR ES SALAAM

    TANZANIA ni moja ya nchi zilizohudhuria mkutano wa 15 wa kimataifa baina ya China na nchi jirani na nchi marafiki katika mji wa Nanning kuanzia Septemba 12 hadi 15 mwaka huu.

    Katika mkutano huo,Tanzania ilihudhulia kama mojawapo ya nchi rafiki wa China iliyoalikwa kushiriki na ujumbe kutoka nchini uliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ,Balozi Seif Ali Idd pamoja na wafanyabiashara 23 walioratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)

    Kati ya nchi zilizoshiriki ni pamoja na Ufilipino ,Singapore,Malaysia,Tahland na Indonesia huku kukifanyika kongamano lilliloshirikisha wafanyabiashara wa China 50 wenye nia ya kufanya biashara nchini.

    Katika maonesho hayo mazao 10 kutoka Tanzania yalipata biashara katika masoko ya China ambapo wafanyabiashara na wakulima wataungana na kuwa timu itakayohakikisha hatua hiyo inafanikiwa kwa lengo la kukuza uchumi.

    Mazao yanayohitajiwa kwa wingi katika soko la China ni Korosho, kahawa,mbaazi, Choroko, dengu, Chai, Tangawizi, Asali na mhogo ambazo kati yao yalioneshwa kwenye maonesho hayo pamoja na madini na bidhaa nyingine na fursa za utalii na mambo mengine.

    Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE,aliyeshiriki maonesho hayo anasema watanzania wanatakiwa kujipanga kukamata soko la mazao hayo huku ,Novemba mwekezaji kutoka China mwenye nia ya kuwekeza katika kiwanda cha kusindika mihogo atatembelea nchini kuona maeneo na fursa zilizopo.

    Anabainisha kuwa lengo la mwekezaji huyo ni kujenga viwanda vya kuchakata mihogo ili bidhaa zake ziweze kuuzwa China kwani nchi hiyo inahitaji wanga katika kutengeneza nguo na dawa ,Mafuta (ethanol) keki na bidhaa mbalimbali hivyo baada ya kuwasili mamlaka hiyo itamtembeza maeneo mbalimbali kuona fursa zilizopo.

    Alibainisha kwa Korosho kuna mfanyabiashara anataka tani 3,000 ya korosho zilizosindikwa ambazo akitokea mfanyabisahar wa kuzipeleka atanunu kwa gharama yeyote.

    Katika Kahawa zilizochakatwa kuna wanunuzi pia kutoka kampuni 10 ambazo zimeonesha nia ya kununua pamoja na maharage na kualika watu wanaotaka kuwekeza katika mazao hayo kuwasiliana na TANTRADE.

    Anasema Mbaazi ni zao jingine ambalo China wanataka kununua kiasi chochote kinachozalishwahuku choroko na Tangawizi zikihitajika zilizoongezwa thamani na kutaka wafanyabishara kuchangamikia pamoja na asali.

    Kutokana na fursa hiyo,wazalishaji wa bidhaa hizo waende Tantrade kuona namna wanavyoweza kuzalisha na kusafirisha kupeleka China

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako