• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kusaidia Tanzania awamu ya pili Utafiti kutokomeza Malaria

  (GMT+08:00) 2018-12-07 10:02:47

  Na Theopista Nsanzugwanko,DAR ES SALAAM

  TANZANIA ni miongoni mwa nchi za Afrika inayokabiliwa na maradhi na vifo kutokana na ugonjwa wa Malaria, ili kukabiliana na ugonjwa huo hivi karibuni imezinduliwa awamu ya pili ya mradi wa utafiti wa kupambana na malaria nchini kwa lengo la kupunguza maradhi na vifo vinavyosababisha na ugonjwa huo.

  Mradi huo kwa kushirikiana na China,Tanzania itanufaika na mikakati iliyosaidia China kutokomeza ugonjwa huo katika awamu hiyo ya pili ya utafiti.

  China ambayo ni nchi inayoendelea kwa kasi ikiwa inashika nafasi ya pili kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani imefanikiwa kukabili ugonjwa wa malaria katika miaka mitatu iliyopita kwani walikuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 30 lakini sasa wameutokomeza kwa asilimia 100 na hawana mgonjwa hata mmoja.

  Kutokana na mafanikio hayo,wataalamu wa Afya nchini China kwa kushirikiana na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI) wameanza awamu ya pili ya mradi wa utafiti wa kutokomeza ugonjwa huo nchini.

  Inaelezwa kuwa maambukizi ya malaria nchini yamepungua kutoka asilimia 14.5 hadi kufika asilimia saba, hivyo kwa ushirikiano huo timu ya afya inakwenda kwa jamii kuwapima na kuwapa matibabu na ndiyo sababu ya maambukizi kupungua kutoka wastani wa asilimia 80 mpaka kufika asilimia 20 kwa sasa.

  Akizindua mradi huo, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Faustine Ndugulile anasema mradi huo wa awamu ya pili unatoka kwenye utafiti na kuanza kwenye utekelezaji kisha kuangalia matokeo yake,kwani maambukizi mapya ya malaria yamepungua kufikia asilimia 62 na vifo vikifikia asilimia 75.

  Anasema nchi za Afrika zina kiwango kikubwa cha maambukizi pamoja na vifo vitokanavyo na malaria lakini kwa ushirikiano na China, Tanzania itatokomeza ugonjwa huo kama ilivyo kwa China.

  Daktari mtafiti Kiongozi wa mradi huo Tanzania, Prosper

  Chaki anayeshughulikia magonjwa yanayoambukiza anasema awamu ya kwanza ya mradi waliangalia njia bora za kuteketeza malaria ambao ni moja ya magonjwa yanayoathiri watanzania.

  Anasema China wana mbinu zao katika mazingira ya nchini hivyo wamekuwa wakiangalia njia nzuri ya kutumia kwa kukuangalia miundombinu, kiwango cha maambukizina maambukizi yaliyopo.

  Anasema utafiti wa awali waliijikita katika vijiji vya Ikwiriri, Chumbi na Mhoro vilivyopo wilaya ya Rufiji kwa maambukizi kupungua toka asilimia 80 hadi kufika asilimia tano.

  Anasema watatumia dola 600,000 katika awamu hiyo ya pili ya mradi huo ambazo zinafadhiliwa na taasisi ya Bill and Melinda.

  Mwakilishi wa taasisi ya Bill and Melinda, Dina Yang anasema licha ya jitihada kubwa zinazofanyika katika masuala ya afya, bado malaria ni tishio ulimwenguni na zaidi katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Anasema taasisi hiyo inashirikiana na wadau wa malaria ikiwemo taasisi ya ifakara pamoja na mpango wa taifa wa kudhibiti malaria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako