• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaongoza kwa uwekezaji wa mitaji Tanzania kwa zaidi ya Dola za Marekani Bilioni tano

  (GMT+08:00) 2018-12-11 09:47:28

  Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

  CHINA inaendelea kuongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania kwa zaidi ya dola Bilioni 5.8 Duniani katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017.

  China ina miradi 723 ikitoa ajira 87,126 kwa thamani ya dola Milioni 5 962.74,ikifuatiwa na Uingereza yenye miradi 936 iliyozaa ajira 274,401 kwa thamani ya dola Milioni 5,540.07 na Marekani ikiwa na miradi 244 iliyozalisha ajira 51,880 kwa thamani ya dola Milioni 4,721.15.

  Katika Ukanda wa Afrika Mashariki nchi inayoongoza kwa mitaji ni Kenya ikishika nafasi ya saba kwa kuwa na mitaji kwa kuwa na miradi 508 iliyozalisha ajira 50,713 yenye thamani ya dola Milioni 1,676.22.

  Tawimu hizo za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zimebainisha kuwa China inaendelea kuwa nchi yenye lengo la kuwekeza zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, viwanda, utalii, Ujenzi, Teknolojia ya Mawasiliano na nyinginezo .

  Katika kuonesha nia ya uwekezaji,wiki iliyopita wawekezaji 17 kutoka nchi hiyo wamefika nchini kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe anabainisha kuwa wakati wa mkutano wa wawekezaji 17 na wawakilishi wa kampuni za kitanzania 136 kuwa baada ya mazungumzo na taasisi za uwekezaji nchini mwekezaji huyo amejitokeza kuonesha nia ya kujenga kiwanda.

  Anasema wawekezaji hao baada ya kuangalia mazingira ya uwekezaji nchi wameelekea nchini Kenya na Ethiopia kwa ajili hiyo na baadaye kufanya maamuzi ya nchi gani kuwekeza lakini katika Korosho mwekezaji huyo amefanya maamuzi.

  Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda anawaalika wafanyabiashara kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani za bidhaa za kilimo ikiwemo Korosho kwa kujenga viwanda.

  Alisema Tanzania ina uwezo wa kuzalisha tani 275,000 za Korosho lakini viwanda vilivyopo vina uwezo wa kubangua korosho 127,000 lakini vingi havifanyi kazi na sasa kuwa na uwezo wa kubangua korosho 30,000 pekee.

  Kakunda anataka kampuni za China kuchangamkia fursa hiyo ya uwekezaji kwa kujenga viwanda vya kubangua korosho kwani China ni nchi inayoongoza kwa kuwekeza mitaji mingi nchini hivyo waendelee kuwekeza ili nchi ipunguze kuagiza zaidi bidhaa toka China bali bidhaa nyingine ziuzwe katika soko la China nan chi nyingine duniani.

  Anasema serikali iko tayari kusaidia wawekezaji kukabiliana na changamoto mbalimbali huku wakiweka mazingira bora ya uwekezaji kwa kupunguza kodi katika rasilimali za viwandani pamoja, Guarantee ya usalama wa viwanda na nyinginezo.

  Awali, Balozi wa China nchini Tanzania Bibi Wang Ke alisema ujio wa wawekezaji hao nchini Tanzania ni katika utekelezaji wa makubaliano ya mkutano wa Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) uliofanyika septemba mwaka huu katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda.

  Anasema Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji ambazo wawekezaji hao wanaweza kutumia ikiwa pamoja na kuwepo mazingira bora ya uwekezaji kutokana na sera bora zilizowekwa na serikali.

  Naye,Mwenyekiti wa baraza la kukuza uhusiano kati ya nchi zinazoendelea kutoka China, Lv Xinhua anabainisha kuwa ujio wa wawekezaji hao ni katika kukuza ushirikianbo baina ya Tanzania na China kwenye kujenga uchumi kwa kukuza mahusiano kwa serikali na sekta binafsi.

  Katika uwekezaji wamelenga kufanya kazi na kampuni za ndani katika Nyanja tofauti ili kuhakikisha inakuwa na faida kwa pande mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako