• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikutano miwili na uongozi wa china machoni pa mtaalam wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-28 09:18:15

    Mikutano miwili ya mwaka nchini China, ya bunge la umma la China na Mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa, inawapatia fursa wageni waalikwa kujifunza kutoka China mifumo ya utawala na usimamizi wa Chama.

    Mwandishi wetu wa Nairobi Ronald Mutie amezungumza na bwana Cavince Adhere mmoja wa wasomi kuhusu ushirikiano wa China na Afrika kuhusu matarajio na ufahamu wake kuhusu mikutano hiyo na mfumo wa kisiasa wa China.

    Hii hapa ripoti yake.

    Mikutano hiyo ndio kusanyiko kubwa la viongozi wa chama cha kikomonisti cha China CPC kila mwaka chini humo.

    Mbali na viongozi wa China pia wageni na waandishi wa habari kutoka kote duniani hualikwa kushuhudia mfumo wa kisiasa wa China.

    Nchini Kenya nimekutana na mmoja wa wasomi wa maswala ya ushirikiano kati ya China na Afrika bwana Cavince Adhere.

    Anaona kuwa pamoja na mambo mengine mkutano huu utaangazia ushirikiano wa China na nchi za kigeni huku maafisa wakijadili njia bora za kuendeleza mawasiliano na dunia.

    "Mkutano huu unatoa fursa kwa mfumo wa utawala wa China, wataalam na wasomi kuangalia upya mambo yaliopata ufanisi na yale ambayo hayajafanikiwa kwenye utungaji wa sera. Wanajadili pia mahusiano ya China na nchi nyingine kote duniani. Kama unavyojua sera ya China kuhusu Afrika inaendelea kuwa ya kina zaidi na tumeona ikifanikiwa kwenye majukwaa tofauti kama vile Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC. Tumeona pia maonyesho ya kwanza ya kuagiza yaliyofanyika Shanghai ambayo yatasaidia kukuza mauzo ya nje ya Afrika nchini China."

    Ndani ya kizazi mimoja tu China imefanikiwa kuondoa mamilioni ya watu kwa umaskini na kuwa na jamii yenye ustawi.

    Kulingana na ripoti ya Baraza lakitaifa ya Kupunguza Umasikini na kuleta Maendeleo mwaka huu serikali inapanga kuondoa umaskini kwa kaunti 330 na kaunti 70 mwaka 2020.

    Mafanikio haya ya kama anavyosema bwana Adhere yamechangiwa na kuwepo kwa mfumo wa kufanya kwa haraka maamuzi na utekelezaji.

    "Ni rahisi kufanya uamuzi nchini China na rahisi kutekeleza. Ni jambo zuri kuwa na mfumo unaofanya kazi ambao unaweza kufanya mambo kusonga mbele. Mfumo wa China umefanikiwa nchini humo. Nadhani chaguo bora zaidi ni Kwa nchi za Kiafrika kuchunguza na kuelewa, ni nini wanaweza kufanya vizuri kuongeza kasi ya maamuzi ambayo inathiri maisha ya watu. Tunahitaji kuangalia baadhi ya mifumo inayofanya kazi na inayoungwa mkono na serikali kuu na ambayo inaonekana kuwasaidia watu wa China ni kitu tunachohitaji Afrika."

    Mikutano hii miwili inafanyka wakati pia China ikiendelea kuongeza ushirikiano wake na Afrika katika kupambana na rushwa na usimamizi wa raslimali za umma.

    Mwaka 2018 serikali ilianza kutekeleza sheria ya kupiga marufuku biashara ya aina yoyote ile inayohusisha pembe za ndovu ili kuziba mwanya unaotumiwa na wawindaji haramu na wafanyabiashara, lengo la jumla likiwa ni kusaidia kuhifadhi wanyapori wa Afrika ambao ni tegemeo kuu la mapato ya kitalii.

    Bwana Adhere anasema anatarajia nchi za Afrika kuendeela kushirikiana na China kwenye swala hili.

    "Maeneo muhimu ambayo nadhani Afrika inaweza kujifunza ni katika masuala kama kupambana na ufisadi, serikali ya China imekuwa na ufanisi sana katika kusimamia rasilimali za umma.Tumeona viongozi wakiwekwa jela bila kujali nafasi yako katika jamii."

    Zaidi ya maafisa 3,000 wanatarajiwa kwenye mkutano huu wakijumuisha watunga sera wa ngazi za mikoa na washauri wa kisiasa kujadili maswala ya kijamii ya kiuchumi katika mwaka uliopita na kupanga mikakati ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako