• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Umma na mustakabali wa FOCAC

    (GMT+08:00) 2019-03-04 08:45:28

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    MWEZI Septemba mwaka jana, 2018, viongozi mbalimbali na Marais wa nchi za Afrika walikutana na viongozi wa China, chini ya uenyekiti was Rais Xi Jinping, jijini Beijing.

    Ni katika Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika, FOCAC, ambapo pande hizo mbili zilijadiliana na kufanya makubaliano juu ya mambo mbambali ya ushirikiano katika miaka mitatu ijayo.

    Mkutano huo uliongozwa na Rais wa China kwa kushirikiana na mwenyekiti mwenza, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

    Mkutano kama huo ulifanyika mwaka 2015, jijini Johannesburg, Afrika Kusini na hufanyika kila baada miaka miaka mitatu. Mwaka 2021 utafanyika jijini Dakar, Senegal.

    Miezi mitano baada ya mkutano huo muhimu kukaa, Bunge la Umma la China linaanza vikao vyake kuanzia Machi 5.

    Chombo hiki muhimu cha maamuzi kinapoanza shughuli zake, ambayo pamoja na mambo mengine kinashughulikia na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu ushirikiano wake na mataifa mengine lakini pia ndicho chenye jukumu la kupitisha maazimio mbalimbali ya serikali.

    Ikumbukwe kuwa mwaka jana katika mkutano huo wa FOCAC, Rais Xi alitangaza maeneo mapya ya ushirikiano wake na nchi za Afrika.

    Maeneo hayo ni pamoja na uimarishwaji wa ushirikianio katika sekta ya afya, elimu, miundombinu, biashara na uwekezaji na ulinzi na usalama.

    Pia, Rais Xi alitangaza kuwa nchi yake itatoa fedha takribani Dola za Kimarekani bilioni 60 kwa nchi za Afrika, ambayo itakuwa ni sehemu ya msaada kwa bara la Afrika na mkopo wenye riba nafuu.

    Zaidi, China pia ilitangaza kuwa itasamehe sehemu ya madeni ambayo inadai baadhi ya nchi za Afrika ambazo zinaoneka kuwa na uwezo mdogowa kulipa.

    Vilevile, nchi hiyo ya pili kwa uchumi mkubwa duniani iliweka bayana nia yake ya kuendeleza jitihada zake kuhakikisha kuwa mradi wa Ukanda Mmoja, Njia Moja unapata msukumo mpya na unatekelezea kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa kwa manufaa ya bara la Afrika, China na dunia nzima kwa ujumla.

    Ukanda Mmoja, Njia Moja, ni mradi wa mabilioni ya dola za Kimarekani ulioasisiwa na Rais Xi kuunganisha bara la Asia, Ulaya na Afrika ili kurahisisha mawasiliano na namna ya kufanya biashara na uwekezaji katika kanda hizo.

    Bunge la Umma la China likiwa linaanza vikao vyake, nchi za Afrika ambazo kimsingi ni moja ya wadau muhimu katika mambo yote ya msingi ya China, zinaguswa moja kwa moja na maazimio ya chombo hiki.

    Maazimio yaliyofikiwa katika mkutano FOCAC, ni moja ya mambo ambayo kivyovyote vile yatakuwa mambo ya msingi yatakayojadiliwa na Bunge la Umma la China ambayo pamoja na manbo mengine, kinahusika na kupitisha bajeti ya serikali na kujadili ushirikiano wake na mataifa mengine.

    Ushirikiano wa China na nchi za Afrika, ni moja ya mambo muhimu ambayo kivivyote vile lazima utapewa kipaumbele cha juu sana katika mkutano huu.

    Nchi za Afrika, kwa mantiki hii, ni dhahiri kuwa zinafatilia kwa ukaribu sana mkutano huu kwa sababu kuu mbili.

    Moja ni kwamba jambo lolote linahusu China ambayo kimsingi ni mshirika namba moja wa Afrika katika biashara na uwekezaji lazima liguse bara hilo.

    Lakini jambo la pili na la muhimu ni kuwa maazimio yote yaliyofikiwa katika mkutano wa viongozi wa afrika na China Septemba mwaka jana lazima yaletwe mbele ya chombo hiki ili kujadiliwa na kupitishwa.

    Kimsingi, Afrika, mbia mkubwa wa China katika mambo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii inatizama mkutano huu kama sehemu muhimu ambayo itatoa mwanga na matumaini katika nyanja mbalimbali ambazo tayari zimefikia makubaliano ya ushirikiano.

    Mwisho--

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako