• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CPC na CPPCC taswira ya Maendeleo China na mahusiano baina ya Afrika na Ushirikiano kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-03-04 08:47:46

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    MACHI 3 mpaka 15 mwaka huu kunafanyika Mikutano Miwili Mikubwa kwa mustakabari wa nchi ya China ambapo serikali itatoa ripoti ya utendaji kazi wake, mafanikio na mipango yake kwa mwaka huu.

    China inayoongozwa na Chama cha Kikomunisti cha CPC kinachoongozwa na Rais wake Xi Jinping inaelezwa kuwa taifa la pili duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa, wiki hii unafanyika mkutano wa pili wa Bunge la 13 la Umma la China.

    Mkutano wa pili wa Baraza la Mashauriano la Kisiasa la awamu ya 13 la China na Mkutano wa pili wa Bunge la awamu ya 13 la Umma la China itafanyika Beijing, China.

    Mwezi kama huu kila mwaka China inafanya mikutano hii muhimu ya kisiasa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya nchi inayoshirikisha wajumbe zaidi ya 3,000.

    Mikutano hiyo inayoripotiwa na vyombo vya habari mbalimbali duniani kiasi ambacho kunakuwa na sehemu maalum kwa ajili ya waandishi wa habari ili waweze kutoa habari ya kinachoendelea katika mikutano hiyo inayofanyika kwa zaidi ya siku 10.

    Mkutano wa Bunge la Umma la China NPC na mkutano wa kwanza wa awamu ya 13 ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China CPPCC, inayojulikana kwa pamoja kuwa ni "Mikutano Miwili" mwaka jana ulifanya mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

    Mkutano huo unaosubiriwa kwa hamu na raia wa China, Afrika na Duniani, mbali na mabadiliko ya katiba inaangalia yale yaliyoahidiwa kwa miaka iliyopita pamoja na malengo ya serikali kwa mwaka huu na mikakati mingine katika ujenzi wa nchi hiyo na ushirikiano wa kimataifa.

    Katika utendaji wa serikali ya nchi hiyo kulikuwa na mapendekezo kwa ajili ya utendaji wa serikali kwa mwaka huu, kwa pato la ndani kukua kwa asilimia 6.5, kiwango cha bei ya bidhaa kitapanda kwa asilimia tatu, huku nafasi mpya za ajira zikiongezeka kwa zaidi ya milioni 11.

    Hii ni sehemu kubwa ya wananchi wanaotaka kusikia katika ukuaji wa pato la ndani la Taifa (GDP), bei za bidhaa na nafasi za ajira kufikia milioni 11 hivyo kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira.

    Mwaka jana, serikali ya China ilidhamiria katika maeneo ya mijini watu wenye ukosefu wa ajira kuwa kwa asilimia 5.5, huku wakitilia mkazo kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja na uchumi kwa ujumla, katika kuonesha dhamira ya kweli ya maendeleo kwa nchi hiyo pamoja na nchi nyingine hususan za Afrika, China kupitia mradi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja unaotarajiwa kuzinufaisha baadhi ya nchi za Kiafrika.

    Baraza la Mashauriano la Kisiasa la China, limeeleza kuwa mradi huo wa mabilioni ya dola za Kimarekani unatarajiwa kufaidisha nchi za Tanzania, Kenya pamoja na nchi zingine za Afrika Mashariki.

    Nchi zingine za Afrika zitakazonufaika na mradi huo ni Ethiopia, Djibouti na Misri kwa kuwekeza dola za Marekani takribani bilioni 60, hivyo hapa nchi za Afrika zinazonufaika na fedha hizo na zisizonufaika kuangalia iwapo wameingizwa katika miradi stahili.

    China katika mipango yake imeweka kufikia mwaka 2020, kufanikiwa kuondoa umasikini hivyo ikiwa imebaki siku chache, serikali itaeleza mafanikio yake katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

    Mkutano wa Bunge wa mwaka uliopita, ulipitisha mabadiliko ya Katiba iliyoondoa ukomo katika nafasi ya urais pamoja kufanya uchaguzi wa viongozi wakuu wa nchi hiyo, kutokana na Baraza la Mashauriano la Kisiasa mwaka jana kutoa ripoti ya kazi kwa vipindi vilivyopita, ilieleza kufanya tathmini ya mfumo wa mahusiano na mataifa mengine na kuangalia namna ya kuboresha mahusiano hayo ili yawe bora zaidi.

    Hivyo nchi za Afrika na nyingine duniani zinatarajia maamuzi ya serikali katika nyanja hiyo ya mahusiano huku raia wa China wakitarajia kulenga kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja hivyo kuondokana na umasikini.

    Sera ya kuimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi zingine duniani, serikali imekuwa ikisisitiza usawa na faida kwa wote katika njia zake za ushirikiano na mataifa makubwa na yale machanga mengi yakitokea Afrika.

    Kutokana na dhana yake ya kufika mbali kimaendeleo na kusimamia maslahi ya nchi hiyo katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii, Bunge la Umma la China lilimpitisha kwa umoja wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako