• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namna China ilivyojidhatiti kuboresha uchumi katika mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-03-05 15:59:36

    Na Deogratius Kamagi, Beijing

    SERIKALI ya China, Jumanne iliwasilisha mswada wa wa bajeti na ripoti ya kazi inazotarajia kuzifanya mwaka 2019 huku ikiweka vipaumbele katika ukukuza uchumi, biashara ajira, kujenga miundombinu pamoja na kuendeleza ushiriakno wa kimataifa.

    Mswada huo ambao ulienda sambamba na ripoti ya utekelezaji wa kazi za serikali ya China kwa mwaka 2018 ulisomwa katika ufunguzi wa kikao cha pili cha bunge la 13 la Umma la china.

    Akisoma ripoti ya utekelezaji wa kazi za serikaliya China kwa mwaka 2018 pamoja na mswada wa bajeti ya mwaka 2019 katika kikao ambacho pia kilihudhuriwa na Rais Xi Jinping, Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang alitumia wasaa huo kuhakikishia dunia kuwa uchumi wa taifa hilo upo imara na kwamba katika mwaka 2019, wanatarajia pato la taifa kukua kwa wastani wa asilimia 6 hadi 6.5.

    Alisema serikali hiyo inatarajia kutengeneza ajira milioni 11 kutoka katika sekta ya viwanda ambavyo pia vimewekewa mkazo mkubwa katika mipango ya mwaka huu.

    "Msisitizo mkubwa pia umewekwa katika ujenzi wa viwanda, kupunguza kodi katika biashara ndogo na za kati hivyo kusaidia kupunguza tatizo la ajira mijini na vijijini,"alisema waziri mkuu huyo.

    Utekelezwaji wa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja pia haujasahaulika katika mipango ya mwaka huu kwani serikali imethibitisha kuendelea na juhudi za kufanikisha miradi hiyo kwa lengo kuu la kukuza biashara na ushirikiano wenye kuongeza tija baina na China na mataifa mengine ambayo yatapitiwa na mradi huo.

    Lengo la pendekezo hilo ni kufufua njia Hariri ya kale ya baharini ili kukuza biashara baina ya nchi za Afrika, Ulaya, Asia na China pamoja na kuzisaidia nchi washirika kukua kiuchumi.

    Tanzania ni moja ya nchi zitakazonufaika na mradi wa Ukanda Mmoja Njia Moja kupitia mipango ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo na mji wa viwanda mkoani Tanga hivyo kuimarisha ushirikiano hasa katika Nyanja za uchumi.

    Mapema siku ya jumatatu, Msemaji wa bunge la Umma la Zhang Yesui aliwaambia waandishi wa habari kuwa China haina mpango wa kuweka masharti kandamizi ambayo yatazisababishia nchi shiriki madeni na kwamba mradi huo itanufaisha pande zote.

    Kwa upande wa miundombinu ndani ya China, serikali hiyo imeongeza bajeti ya kujenga miundombinu kufikia Yuani za China bilioni 577.6 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 200 za Tanzania) kutoka Yuani bilioni 537.6 (sawa na shilingi trilioni 188 za Tanzania) kwa mwaka jana.

    Akizunguzia biashara za kimataifa, Waziri Mkuu huyo alisema wataendelea kuboresha mazingira ili kuvutia wawekezaji nje na ndani ya china.

    "Tutajitahidi kupunguza muda wa kukamilisha hatua za kiforodha hivyo kuvutia biashara nyingi zaidi, lakini pia kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na makampuni binafsi," alisema.

    Kuhusu utekelezaji wa mipango ya mwaka 2018, kiongozi huyo alitaja mambo kadhaa waliyofanikiwa kuyafanya ikiwemo kampeni dhidi ya uchafuzi wa mazingira, kongeza ajira milioni moja na laki nne pamoja na kuongeza kasi ya katika kusajiri biashara mpya.

    Alisema kwa sasa wana uwezo wa kusajiri biashara mpya 18,400 kwa saa moja na kwamba hiyo ni kasi nzuri ambayo wamejipanga kuendelea nayo kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako