• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchina yakanusha madai ya kurejesha utawala wa kiukoloni Afrikani

    (GMT+08:00) 2019-03-08 18:01:29
    NA VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    UCHINA umekanusha madai kwa inapanga kurejesha utawala wa kibeberu afrikani kupitia mpango wake wa kujenga barabara unaojulikana kama "Belt and Road Initiative" (BRI).

    Waziri wa Mambo ya Nje bwana Wang Yi akizungumza na waandishi wa habari leo (Ijuma) mjini Beijing, alionya kuwa uvumi huo unaenezwa na wale hawapendezwi na maendeleo ya haki ulimwenguni.

    Bwana Wang aliongezea kuwa ushirikiano wa Uchina na nchi za Afrika umejengwa juu miundo misingi wa urafiki wa kitamaduni ulioanza kana za kale na ni ya faida ya pande zote.

    "Kumekuwa na uvumi hapa na pale kuwa Uchina unarudiha utawala wa kiukoloni kule Afrika kupitia miradi tunayofanya pamoja chini ya BRI na huu ni uwongo mtupu, uhusiano wetu ni wa kufaidi pande zote na ina maelewano wa ndani sana," Waziri Wang aelezea.

    Kulingana na bwana Wang, mpango wa BRI si mtego wa deni kwa nchi wanachama ilhali ni hatua ya kuhakikisha kuwa Uchina umechangia pakuu kwenye uchumi wa dunia.

    Alifichua kuwa zaidi ya nchi mia moja na mashirika ya kimataifa ishirini na sita yametia sahihi kujiunga na mradi huo wa ulimwengu.

    "Mradi wa BRI ni moja za njia ambazo nchi yetu unajaribu kuleta nchi za kigeni pamoja na kuchangia kwa uchumi wa ulimwengu na si chochote kuhusu mtego wa kideni," asema bwana Wang.

    Nchi ya Kenya imefaidika sana na mpango huo wa BRI kupitia ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Nairobi kulingana na Waziri Wang akiongezea kuwa kupitia ujenzi huo unaojulikana kama "Standard Rauge Railway", Kenya imefaulu kupata nafasi za ajira elfu hamsini kwa wenyeji na mia tisa kwa watu wa kichina.

    "Uchumi wa nchi ya Kenya umeimarika sana kupitia ujenzi wa reli wa Mombasa na Nairobi na kupata ajira elfu hamsini kwa wakenya na mia tisa kwa wachina," alisema Waziri.

    Kuhusu kongamano wa ushirikiano wa mwaka jana ulioleta viongozi tofauti kutoka Afrika, bwana Wang alisisitiza kuwa wataendelea kushauriana wakitimiza mambo waliokubaliana kama jinsi ya kuthibiti uhusiano.

    Waziri Wang alionya kuwa uhusiano wa Uchina na Merikani utabaki wa ushirikiano pekee na lazima uwe wa kulinda uhuru na mpaka wa wachina.

    Aliongezea kuwa serikali ya China itaendelea kulinda haki halali za wachina kibiashara popote ulimwenguni.

    "Serikali haitakubali wachina ambao wanafanya biashara katika nchi za nje watishwe kwa njia yoyote na ni majukumu yetu kuhakikisha kuwa haki na maslahi ya wachina wote imeheshimiwa," aonya bwana Wang.

    Alipuuzilia mbali pendekezo la Uchina kutohusisha Merikani kwenye uchumi wake akidai kwamba itakuwa kama kukosa kufuata mwanya ambao umeonekana kupitia mazungumzo za awali akisisitiza kuwa hamu ya nchi hizo mbili ni ya namna isiyoweza kutengwa.

    Uchina itakapo sherekea kumbukumbu ya miaka sabini mwaka huu, sera za kidiplomasia nchini zimeanzishwa na utamaduni mzuri na kipengele tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako