• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha Utamaduni wa China na Tanzania chafanya maonesho ya sanaa yenye jumbe za umkomboa mwanamke

    (GMT+08:00) 2019-03-12 08:58:08

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    MWAKA 2015 kilizinduliwa kituo cha kwanza cha utamaduni wa China katika ukanda wa Afrika Mashariki kilichopo jijini Dar es Salaam, Tanzania. Wakazi huo, Aliyekuwa balozi wa China nchini Tanzania Lv Youqing na waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda walishiriki katika uzinduzi wa jukwaa muhimu la kuzidisha mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Tanzania, na kitatoa mchango zaidi katika kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati yao.

    Mbali na mambo mbalimbali ya utamaduni baina ya nchi hizo mbili yanayofanyika kwenye kituo hicho, kimewakaribisha wasanii wa kike wa kitanzania kuonesha kazi zao za mikono ambazo zinaelezea maisha halisi yaliyopo katika jamii katika maonesho maalum ya kumuenzi mwanamke.

    Katika Maonesho hayo wametumia jumbe za kisanaa kueleza changamoto na suluhisho kwa wanawake, hivyo wasanii wa kike nchini wametakiwa kupepeleka kazi zao zinaoeleza maisha halisi ili kutoa ujumbe.

    Mkurugenzi wa kituo hicho nchini, Gao Wei alisema hayo wakati wa ufunguzi wa maonesho yajulikanayo kama "Women's Visual Art Exhibition" yanayofanyika jijini Dar es Salaam kwa wiki nzima kuanzia Ijumaa iliyopita hadi Machi 15, mwaka huu.

    katika maonesho hayo yanayoendelea katika kituo hicho yanaonesha jinsi jamii ilivyo na kuwaomba Watanzania na wasanii kwa ujumla kwenda kujifunza mambo mbalimbali kupitia maonyesho hayo.

    Mratibu wa Maonesho hayo, Ruth Sabai alisema maonesho hayo yenye kauli mbiu "tambua thamani yako" yameandaliwa kwa ajili ya kusherehekea siku ya wanawake duniani ina wasanii 15 kati ya hao wanaume ni wanne tu.

    Sabai anasema kwa kutumia sanaa zinazungumzia vitu mbalimbali ikiwahusisha wanawake kujua thamani yao ikiwa ni pamoja na majukumu yao ya kila siku katika jamii.

    Anasema moja ya sanaa zilizopo katika maonesho hayo moja ya sanaa inaeleza utafiti umeonesha kuwa wasichana wengi wanashindwa kusoma wanapokuwa katika siku zao za hedhi,hivyo wanaonesha kuwa hedhi ni jambo la kawaida siyo aibu na jinsi ya kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wasichana

    Msanii Mkazi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Idara ya Sanaa Bunifu, Sufira Kimbokota anasema maonesho hayo ya picha yanawasilisha ujumbe kwani sanaa ina nguvu katika kuelimisha jamii.

    Anasema kupitia sanaa aliyoichora inaonesha umiliki wa ardhi ambao katika familia nyingi mwanaume ni mmiliki wa ardhi hata kama mwanamke amechangia katika upatikanaji wa ardhi hiyo,

    Hivyo sanaa hiyo inamtaka mwanamke ajitambue kuwa ana haki sawa na mwanaume. Anabainisha kuwa maonesho hayo yamefadhiliwa na Kituo hicho cha Utamaduni wa China pamoja na Nafasi Art Space na Vipaji Gallery.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako