• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tutaendelea Kushirikiana na Tanzania, Balozi Wang asisitiza

    (GMT+08:00) 2019-03-15 08:41:07

    Tutaendelea Kushirikiana na Tanzania, Balozi Wang asisitiza

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    BALOZI wa China nchini Tanzania Bi Wang Ke amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Kabudi na kumhakikishia kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo. `

    Mazungumzo hayo yaliyofanyika jijini Dodoma, Tanzania jana, Machi 13, 2019, pamoja na mambo mengine yalijikita katika ushirikiano na mshikamano wa nchi hizo mbili ambazo mwaka huu zinajiandaa kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kibalozi.

    Balozi Wang pia amewasilisha kwa Waziri Kabudi pongezi kutoka kwa Bw Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China kufuatia Prof Kabudi kuteuliwa Rais John Magufuli kuwa Waziri katika wizara hiyo muhimu katika nyanja ya kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa.

    Aidha Prof Kabudi kupitia kwa Balozi ameshukuru kwa salamu hizo za pongezi alizopokea kutoka kwa waziri mwenzake, Bw. Wang.

    Katika mazungumzo yao, Prof Kabudi na Balozi Wang, wameahidi kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizo mbili.

    Kwa pamoja, wamesisitiza umuhimu wa kuendelea na jitihada za kuimarisha mahusiano ya kisiasa, kijamii, kiuchumi hususan kwenye maeneo la uwekezaji, biashara, utalii na miundombinu.

    Prof Kabudi ametumia fursa hiyo kuishukuru Jamhuri ya Watu wa China kwa misaada ya kimaendeleo wanayoendelea kuitoa na kwamba Tanzania inafurahishwa na Jinsi China inavyounga mkono jitihada zake za kuwaletea wananchi maendeleo na kujenga uchumi.

    Tanzania na China zimekuwa na mahusiano ya kidiplomasia tangu mwaka 1964 na mwaka huu zinatarajia kuadhimisha miaka 55 ya ushirikiano huo.

    Balozi Wang amekuwa Balozi wa kwanza kuonana naProf. Kabudi tangu kuteuliwa kwake kuiongoza Wizara hiyo.

    Kutokana na kuimarika kwa Ushirikiano kwa miaka mingi, China imekuwa ikiongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania kwa zaidi ya dola Bilioni 5.8 Duniani katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017.

    Uhusino wa China na Tanzania uliasisiwa na marais wa kwanza wa mataifa hayo katika miaka ya 1960,--Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Mao Zedong -Tung wa China.

    Hadi sasa Watanzania wanajivunia mengi, ikiwa na ujenzi wa reli ya Tazara, miradi ya viwanda kama vile cha nguo –Urafiki.

    Urafiki wa mataifa hayo mawili, yamejikita katika sekta mbalimbali, zikiwamo biashara, ulinzi na viwanda. Lakini kwa sasa, unazidi kusambaa katika sekta nyinginezo

    Picha:

    Prof Kabudi akiwa katika mazungumzo na Balozi wa China mara baada ya kupokea barua ya pongezi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako