• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Sanya wapanga kuanza kushirikiana na miji mbalimbali ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-26 16:14:13

    Na Deogratius Kamagi, Sanya

    MJI wa Sanya ambao ni maarufu kwa utalii uliopo kusini mwa china katika kisiwa cha hainan umesema unampango wa kuanzisha mashirikiano katika nyanja mbalimbali na miji ya barani Afrika.

    Ushirikiano huo utalenga katika masuala ya maendeleo kama vile biashara, elimu na kukuza sekta ya utalii kwa maendeleo endelevu.

    Hayo yalielezwa jana, Jumatatu na Mchumi mkuu wa tume ya maendeleo na mageuzi Bw Zhao Yiwen wakati wa ziara ya waandihi wa habari 50 kutoka mataifa 34 ya Afrika na 16 kutoka bara la Asia.

    Alisema ushirikiano huo utasaidia pia katika kutekeleza miradi ya Ukanda mmoja njia moja ambayo inahusisha China pamoja na nchi zaidi ya 150 na taasisi na mashirika ya kimataifa yapatayo 29 duniani kote.

    "Ushirikiano huu utasaidia kukuza utalii na kuboresha nyanja nyingine za mashiriakiano baina ya pande zote husika ambapo sote tutanufaika kama ambavyo ilielezwa na Rais Xi Jinping ambaye ndiye muasisi wa mkakati huu," alisema.

    Pia ilielezwa kuwa katika mwaka 2018, Sanya ilipokea jumla ya watalii 801,000 kutoka nchio 59 ambazo zimeondolewa hitaji la viza kwa raia wake ambao watafika kutalii katika mji wa Sanya na kukaa kwa muda usiozidi mwezi mmoja.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na viongozi wa mji wa Sanya, jumla ya watalii milioni 22.2 walitembelea mji huu mwa mwaka jana.

    Katika maelezo yake, mtafiti kutoka kamati ya utalii,utamaduni, redio, televisheni na michezo Bw. Tang Sixian alisema kwa mwaka huu wanatarajia kuongeza idadi ya watalii kwa zaidi ya asilimia kumi.

    "Haya yatawezekana kwani mji huu una vivutio vingi na miundombinu yenye uwezo wa kupokea wageni wengi kwa wakati mmoja," alisema.

    Akitaja sababu mbalimbali zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ikiwemo hali nzuri ya hewa, ulinzi na usalama pamoja na ukarimu wa wenyeji.

    "Tuna hoteli kubwa na za kisasa zenye hadhi za kimataifa zaidi ya 200, usafiri wa uhakika pamoja na huduma zote za kijamii, hivyo lengo la kuwa kivutio kikukwa cha kimataifa linawezekana kabisa" alisema mtaalamu huyo wa utalii.

    Pia, uongozi wa mji wa Sanya umeondoa hitaji la Viza kwa raia kutoka nchi 59 zilizo chini ya mkakati wa ukanda mmoja njia moja ambao watafika kutalii katika kisiwa hiki na kukaa kwa muda usiozidi siku 30.

    "Kwa hiyo mashirikiano na miji ya Afrika itawezesha kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali hivyo kutuwezesha sote kusinga mbele kwa pamoja," alisema Bw Tang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako