• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mafunzo kwa wahandisi wa ujenzi Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-27 09:17:13

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    KAMPUNI ya Ujenzi ya China—"Chinese-Group Six International Limited (GSI)" imeanzisha mafunzo ya miezi mitatu ya kuwaongezea uwezo wahandisi wa ujenzi wa kitanzania.

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa GSI Janson Huang alisema programu hiyo itafanyika nchini Tanzania kwa muda wa miezi miwili na watakaofanya vizuri watachaguliwa kwenda China kwenye Chuo cha Uhandisi na Ufundi Stadi cha Chongqing kwa mwezi mmoja.

    Alisema pia mafunzo hayo yatahusisha elimu kwa njia ya masafa kwakutumia mtandao kutoka kwenye chuo hicho ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza ujuzi mbalimbali kwenye masuala ya uhandisi wa ujenzi.

    "Kupitia elimu kwa njia ya masafa wanafunzi watawezeshwa kupata ujuzi mbalimbali katika masuala ya uhandisi wa ujenzi wa barabara, madaraja, ukaguzi wa viwango vya ujenzi," alisema.

    Kwa mijibu wake, mafunzo hayo yanawezeshwa na serikali ya jimbo la Chongqing ya China, Chuo cha Chongqing na GSI. Wakufunzi wanaotoa mafunzo hayo pia wanatoka katika chuo cha Chongqing.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Aggrey Mlinuka alisema mradi huo utaisaidia Tanzania kuongeza idadi wa wazawa wenye ujuzi wa masuala ya uhandisi wa ujenzi na kuisaidia nchi kufikia uchumi wa kati na viwanda.

    "Nchi yetu bado ina miradi mingi sana ya ujenzi ambayo mingi miongoni yao inatekelezwa na makampuni ya Wachina, hivyo hii ni fursa adhimu kwa wataalamu wazawa kujiongezea ujuzi na kupata fursa ya kutekeleza miradi hiyo ya kuboresha miundombinu ya nchi yetu," alisema.

    Aliongeza kuwa mbali na kubalishana ujuzi wa masuala ya uhandisi wa ujenzi, mradi utazidi kuimarisha uhusiano na urafiki wa muda mrefu uliopo baina ya China na Tanzania.

    Makamu Mkurugenzi wa Chuo cha Chongqing, Bw Xu alisema kuwa chuo hicho kitawawezesha wanafunzi watakaokwenda China kwa mafunzo ya mwezi mmoja tiketi ya usafiri kwenda na kurudi toka China pamoja na malazi.

    "Tutajitahidi kuendelea kutoa mafunzo kama haya ili kuendeleza na kuimarisha urafiki baina ya China na Tanzania," alisema.

    Katibu wa Ubalozi wa China Tanzania, Sun Chengfeng alisema kwamujibu wa takwimu za ripoti zinazotolewa na vyobo vya habari, asilimia kubwa ya wafanyakazi wa kitanzania wana ujuzi mdogo wa kazi wanazofanya.

    Alishauri, ili kufikia uchumi wa viwanda, ambao ndiyo sera ya serikali ya Tanzania kwasasa, ni lazima kama nchi ni lazima iweke mikakati ya kuwekeza katika kupata wajuzi wengi zaidi, ambapo makampuni ya China tayali yamehamasika kusaidia kutoa mafunzo ya kuendeleza ujuzi kwa watanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako