• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dorice Silas Pokela (Tanzania)

    (GMT+08:00) 2019-03-28 14:36:22

    TANZANIA –ZAMBIA RAILWAY (TAZARA)

    Kihistoria nchi ya Tanzania ni nchi iliyopatikana baina ya nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar kuungana mnamo mwaka 1964, nchi ya Tanzania inapatikana Barani Afrika ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki. China iliyopo Barani Asia na Tanzania ni Mataifa yanayoendana katika mfumo wa utawala ambao ni ujamaa, kimsingi urafiki wa kidiplomasia baina ya mataifa haya mawili ulianza miaka mingi sana , takribani miaka 55 iliyopita

    Kupitia urafiki baina ya mataifa haya mawili pamekuwa na matokeo chanya mengi sana ukiwemo mradi wa TAZARA ambao pia huitwa Uhuru Railway" Mradi huu ni wa reli ambao unahusisha 1, 860 kilometa na unaunganisha Dar Es Salaam Tanzania hadi KapiriMposhi Zambia. TAZARA ni ufupisho wa maneno matatu yaani Tanzania-Zambia Railway. Mradi wa TAZARA ulianza mbio zake za kujengwa pale ambapo Rais wa wa Nchi ya Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere alipotembelea Beijing, China Februari mwaka 1965. Mazungumzo ya mradi wa TAZARA yalifanywa na Marais wa pande zote mbili yaani Tanzania na China pia Mh. Mao Zedong kama mwenyekiti.

    Serikali ya China chini ya Ministry of Railway and China Civil Engeneering Constructor Corporation, kwa kipindi cha mwaka 1965-1976 ilifanikiwa kuleta jumla ya wataalamu 50, 000 wakiwemo na wafanyakazi , 30, 000-40, 000 . Na mradi huu uliweza kuwashirikisha waafrika 60, 000 ambao walishiriki katika hatua mbalimbali za ujenzi.

    TAZARA inatoa huduma ya usafirishaji wa mizigo na pia inatoa huduma ya kusafirisha raia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Shukurani ziende pia kwa waendeshaji (utawala) wa mradi huu na serikali yetu ya Tanzania kwa kuweza kuuendeleza hadi hii leo. Kupitia mradi huu tunaweza kufanya biashara ndani ya nchi na hata pia kwenda nchi jirani ya Zambia, hivyo kuongeza kipato cha wananchi wa nchi hizi mbili. Umoja wetu umezidi kudumishwa miongoni mwetu , urafiki unakuzwa kadiri tunavyo changamana, tunapata mawazo mapya na fursa mpya zinaibuka kadiri tunavyozidi kubadilishana mawazo.

    Moja ya picha iliyopo katika jengo moja wapo la Tazara - Dar Es Salaam ikionyesha ramani inayo onyesha ujenzi , sehemu ambazo reli imepita na kuunganisha nchi hizi mbili Tanzania na Zambia

    Hapo juu ni baadhi ya picha za wahasisi wa urafiki baina ya nchi ya China na Tanzania. Katika harakati za kuenzi urafiki baina ya nchi hizi mbili , Tazara –Dar Es Salaam wamechapisha nakala za picha za Wahasisi wa umoja huu unao dumu ili iwe kumbukumbu inayo onekana na kusimulika miongoni mwa raia wote wanaofuata huduma katika eneo husika.

    Tazara –Dar Es Salaam hii ni picha inaonyesha mandhari ya mojawapo ya stesheni katika hali ya ubora kabisa na tulivu inayowezesha kutoa huduma kwa raia wake .

    Picha bora kabisa ya Tazara –Dar Es Salaam ionyeshao ubora wa njia ya reli iliyojengwa karne za nyuma baina ya ushirikiano wa wafanyakazi wa kutoka nchini China na kutoka Afrika mnamo mwaka 1969 -1975, ambapo ujenzi huu ulihusisha takribani wataalam 50, 000 na wafanyakazi 40, 000 kutoka China na pia na 60, 000 kutoka Afrika ambayo bado inatoa huduma hadi hivi leo kama inavyo onekana kwa ufanisi hapo juu.

    Wafanyakazi wa stesheni moja wapo iliyopo katika eneo la TAZARA –Dar Es Salaam wakionyesha kuwajibika kwa ufanisi katika majukumu yao ili kuhakikisha huduma zinazotolewa ni katika ubora na hadhi ya juu.

    Hapo juu ni picha maridhawa inayo onyesha mazingira nadhifu kabisa ya eneo moja wapo katika stesheni ya Tazara -Dar Es Salaam ambalo raia hutumia katika kuingia katika treni tayari kwa safari , kama vile uwepo wa treni zinavyo onekana katika eneo husika tayari kwa kutoa huduma kwa wananchi.

    Hili ni jengo moja wapo la stesheni ya reli ya Dar Es Salaam likionyesha raia wakihudumiwa katika nyanja tofauti, ramani ya reli inayo unganisha Tanzania na Zambia pamoja picha za ukutani za wahasisi , Maraisi na mabalozi wa nchi hizi mbili ili kuenzi matukio rasmi yaliyo tendeka katika nyakati tofauti.

    Picha ikimuonyesha mmoja wa wafanya biashara akifurahia huduma inayotolewa na kufurahia ubora na uhakika wa usafiri kama mandhari ya treni hapo juu inavyoonekana katika ubora wake. (TAZARA –Dar es salaam). " kwa kweli nina furahia huduma hii na kikubwa zaidi ni kuwasili mizigo yangu kwa usalama huko unakoenda, shukrani ziende kwa utawala na serikali ya nchi yetu na nchi ya China kwa kutuletea huduma hii bora". Alisema mfanya biashara huyu .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako