• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchina kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika kuhifadhi wanyamapori

    (GMT+08:00) 2019-04-05 10:28:09

    NA VICTOR ONYANGO

    Uchina umesema utaendelea kushirikiana na nchi za Afrika kulinda wanyamapori na kusema kuwa mchina yeyote anayeishi kwa nchi za nje atakayepatikana akishiriki biashara haramu ya wanyamapori lazima ashtakiwe kulingana na sheria za nchi hizo.

    Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari kutoka Afrika na Asia leo mjini Beijing, mkurungezi mkuu wa mambo ya ushirikiano wa kimataifa katika wizara ya swala ya misitu na nyasi (National Forestry and Grassland Administration) bwana Meng Xianlin alisema kuwa Uchina umeweka mstari wa mbele mambo ya kuhifadhi wanyamapori.

    Aliongezea kuwa uchina unaheshimu sheria na kanunu za nchi za Afrika kuhusiana na kukabiliana na biashara haramu ya wanyamapori.

    "Na mwongozo wa rais Xi Jinping kuhusu kulinda wanyamapori, tutaendelea kushirikiana na nchi za Afrika na nchi zingine ulimwenguni kuhakikisha maisha ya wanyamapori hayako hatari kutokea matendo ya uwindaji haramu," asema bwana Meng.

    Wachina wengi wamekuwa wakishikwa kwa nchi nyingi Afrikani kulingana na uwindaji haramu. Mwezi wa januari mwaka huu, polisi nchini Kenya walikamata na kushtaki wachina watatu waliopatikana na pembe za ndovu, ngozi ya samba na nyama ya mbwa. Tanzania kumekuwa na kesi ya malkia wa pembe za tembo.

    Lakini bwana Meng alielezea wanahabari kuwa Uchina unaendelea na mpango ulioanzisha 2013 nchini Kenya wa kuelemisha wachina wanaoishi nchi za nje umuhimu wa kulinda wanyamapori ili kosa zilizofanyika hapo awali zikome.

    "Wiki jana tumekuwa Kenya na Botswana kwa maswala ya kufunza raia wetu na wenyeji manufaa ya kulinda wanyamapori. Mpango huu tulianzisha mwaka wa 2013 nchini Kenya na mwaka jana tulikuwa kwa nchi kama Tanzania, Uganda, Rwanda kati za zingine," bwana Meng afichua.

    Alipongeza Kenya kwa kuchukua hatau mwafaka wa kutunga sheria na kanuni ngumu za kuadhibu wawindaji harumu.

    "Tulipokutana na wazira wa utalii wa Kenya, bwana Najib Balala, tuligundua kuwa Kenya ina sheria thabiti za kuhakikisha uwindaji harumu umekomeshwa. Huu ni hatua nzuri kwa upande wa kuhifadhi wanyamapori," asema bwana Meng.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako