• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wa Afrika na China wamehimizwa kuendeleza ushirikiano wa Afrika na China kupitia kufanya utafiti

    (GMT+08:00) 2019-04-09 19:04:25

    Na Victor Oluoch, Beijing, China

    China imehimiza wasomi wake na wa Afrika kuendelea kufanya utafiti mbali mbali ambazo zitaimarisha ushirikiano. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi ya utafiti wa China-Afrika leo, mkurungezi wa maswala ya nje katika kamati kuu ya Communist Party of China (CPC) bwana Yang Jiechi alisisitiza kuwa wasomi mbali mbali wanaezasaidia ushirikiano wa watu kwa watu katika China na Afrika.

    "Kupitia uzinduzi wa taasisi huu, wasomi wetu kutoka nyanja mbali mbali kukuja pamoja na kujadiliana na kufanya jinsi tunaeza kuza

    watu kwa watu kubadilishana mambo fulani," asema Bwana Yang.

    Bwana Yang alisisitiza kuwa wasomi hao lazima watumie taasisi huo kuhakikisha kuwa wamepata jinsi maswala Belt and Road Initiative, afya na biashara umefanikiwa.

    Aliongezea kuwa ushirikiano baina ya China na Afrika utaendelea kuwa wa kufaidi pando zote akihakikishia mabalozi waliohudhuria uzinduzi huo kuwa China itaendelea kuheshimu uhuru wao.

    Aliomba nchi za Afrika kuwa wasidanganywe na nchi za magharibi ambazo alisema kuwa hawafurahishwi na ushirikiano wema baina ya China na Afrika.

    "Sisi tutaendelea kuheshimu uhuru wa nchi za Afrika na kuendelea kushirikiana kwa pande zote tukiwa waaminifu kwa chenye tunafanya. Lazima pia tusidanganywe na wale wenye wanataka kuona kuwa ushirikiano wetu umekuwa hafifu," asema bwana Yang.

    Kwa upande wake, rais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano alipongeza China kuendelea kushirikiana na Afrika kwa mnajili wa kuhakikisha kuwa ajenda wa Umoja wa Afrika wa 1963 wa kuwa bara unayo jitawala kibinafsi.

    "China imekuwa rafiki wa kweli wa Afrika na umeendelea kusaidia Umoja wa Afrika kuhakikisha kuwa ajenda 2063 wa kuendeleza utawala binafsi. Nchi mbali mbali pia zinaendelea kufaidika kupitia ushirikiano huu na nina tumaini kuwa ushirikiano huo utaendelea na kuwa wa dhati," asema Bwana Chissano.

    Bwana Chissano pia alikosoa nchi za magharibi kuendelea kuchapisha majarida yanayopotosha Ulimwengu kuhusu swala BRI na ushirikiano wa Afrika na China akieleza kuwa nchi hizo hazitaki maendeleo ya bara la Afrika.

    Alihimiza wataalamu na watafiti kutoka Afrika na China kupata njia mwafaka unaoweza kutumika ili kuhakikisha porojo na mtasamo zinazochapishwa na nchi za magharibu kuhusu BRI umekanushwa na kumalizwa.

    "Kumekuwa na porojo nyingi kuhusu ushirikiano baina ya Afrika na China kwa hivyo ni jambo kuu inayopaswa kuwa kipao mbele na wataalamu wetu wa Afrika na China kuhakikisha mambo kama haya yamekamilizwa," ahimiza bwana Chissano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako