• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jukwaa la Ukanda mmoja, Njia moja kuanza Alhamisi ijayo mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2019-04-19 13:56:10

    NA VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    China itahudhuria jukwaa la pili la ukanda na barabara kuanzia wiki ujao 25-27 kutoka kwa kushinikiza kwake ili kuunganisha nchi na baharini an ardhi kupitia mtandao wa miundombinu na Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Ulaya.

    Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi leo aliambia waandishi wa habari kuwa China inajitolea kuona ufanisi wa mradi wa mpango mkuu pia unaojulikana kama Silk Road Economic Belt.

    Waziri Wang alifichua kuwa maudhui wa kongamano hilo mjini Beijing kuwa ni ushirikiano wa ukanda na Ushirikiano, kuunda shabaha kuwezesha uwezo linalenga kuleta ushirikiano wa ubora chini ya ukanda mmoja, mpango mmoja wa barabara.

    Alisema kuwa nchi kama Kenya, Djibouti, Ethiopia, Misri na Msumbiji zimethibitisha kujitolea kwao kwenye jukwaa ijayo.

    "Uhusiano wetu na Afrika unabaki wa nguvu na wakati unajaribiwa, hadi sasa, nchi kama Kenya, Ethiopia na Misri kati ya wengine zimethibitisha kuhudhuria jukwaa la pili la Ukanda mmoja, Njia moja," afichua bwana Wang.

    Barani Afrika, China inashiriki sana kwa usafiri na nishati na Nigeria, Angola, Kenya, Ethiopia na Zambia.

    Bwana Wang asema kuwa katika kongamano la wiki ijayo, China inatarajia marais 37 na wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 150 na mashirika 90 ya kimataifa.

    Kwa nchi za kiafrika, Kenya imefaidika na mpango Ukanda mmoja, Njia moja kwa njia ya ujenzi wa reli ya milimi 3.2 ya Mombasa-Nairobi na itatumia jukwaa kueleza jinsi uchumi wake umeboresha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako