• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping ataja fursa zilizotokana na utekelezwaji wa wazo la Ukanda mmoja Njia moja

    (GMT+08:00) 2019-04-26 13:33:25

    Na DEOGRATIUS KAMAGI, Beijing

    Rais wa China Xi Jinping amesema jitihada za pamoja za telekezaji mbalimbali katika kukuza uwekezaji na biashara za kimataifa. Juhudi hizo pia zimeelezwa kuchangiza hatua mabalimbali ambazo zimekua zikichukuliwa katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja katika mataifa yote.

    Rais Xi ametoa kauli hiyo leo Ijumaa katika hotuba yake ua ufunguzi wa mkutano wa pili wa jukwaa la Ukanda Mmoja Njia Moja (Belt and Road Forum) linalofanyika kwa siku tatu katika jiji la Beijing.

    Katika hotuba yake, Rais huyo wa taifa la pili kwa ukuaji wa uchumi duniani amesema nchi yake itaendelea kusaidia nchi zinazoendelea ili kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea katika kuikuza biashara na uchumi.

    "Katika hilo, China itaendelea kutoa msisitizao katika vita dhidi ya rushwa ili kuhakikisha malengo yote yanafikiwa kwa wakati. Tunahitaji kufanya kazi kwa pamoja na kuongeza mashirikiano." alisema.

    Katika hotuba yake, rais Xi pia alisisitiza umuhimu wa nchi zinazoendelea kushiriakinana katika sekta za kilimo, afya, biashara, pamoja na kukabiliana na majanga ya dharula na kwamba bado kuna umuhimu wa kuendelea kubasilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya pamoja.

    "China itaendelea kufanya kaz kwa ukaribu na watafiti na wagunduzi wa china kwa kushiriana na watalamu kutoka nchi nyingine, lakini pia tunasisitiza uwepo wa fursa za biashara huria na huru" alisema katika mkutano ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za takribani 150 duniani huku idadi ya washiriki katika mkutano huu ikielezwa kuwa ni zaidi ya 5,000."

    Katika mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mwasilianao Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye amesema mkutano huu utainufaisha Tanzania kwa kiasi kikubwa.

    "Kupitia mkutano huu, tumeweza kukutana na wenzetu kutoka nchi zinazoendelea, tunabadilishana mawazo na uzoefu hasa katika sekta ya miundombinu ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo na ustawi wa taifa lolote lile kiuchumi." alisema.

    "Jukwaa hili limekuja muda sahihi kwani kwasasa tanzania tunajenga miradi mingi ya barabara, na reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kanda ya ziwa ambayo pia inatarajiwa kuunganisha na nchi za Afrika ya kati." aliongeza.

    Inaelezwa kuwa hadi sasa utekelezwaji wa wazo la Ukanda mmoja Njia Moja limeweza kutengeneza nafasi za ajira takribani 300,000 katika nchi zote zinazounga mkono jitihada hizi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako