• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi kutoka nchi za Ukanda mmoja, Njia moja waahidi maendeleo bora

    (GMT+08:00) 2019-04-28 09:59:47

    NA VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    Rais wa China Xi Jinping na viongozi wengine kutoka nchi za Ukanda mmoja, Njia moja wamekubali kuendeleza mpango huo kwa nyanja za juu.

    Akizumgumza na wanahari katika kituo cha maonyesho cha ziwa ya Yangi mjini Beijing, rais Xi alisema kuwa mkutano wa pili wa viongozi leo (Jumamosi) wamekubaliana kuwa nchi zote wanachama zitachanga fedhakwa manufaa ya kukuza maendeleo wa pande zote.

    Viongozi hao wakubali kutoa bilioni 64 kwa jitihadi za kupitisha kile kinachojulikana kama maendeleo bora kwa nchi wanachama wa Ukanda mmoja, Njia moja.

    Kupitia mawasiliano ya pamoja yaliyosomwa na rais Xi, viongozi hao walibainisha kuwa uchumi wa dunia sasa hivi unakabiliwa na fursa zote za kupanua na changamoto zinazoongezeka kwa hivyo kuna haja ya kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili kukabiliana na masuala ya kizazi bora kijao.

    "Tumesisitiza na kuthibitisha ahadiyetu kwa kuhakikisha kuwa tunakabiliwa na changamoto za maendeleo na matokeo yake, tumetia saini ya ushirikiano wa thamani ya dola billion 64," asema rais Xi.

    Aliongezea kuwa viongozi waridhika na maendeleo na fursa zilizofanywa na Ukanda mmoja, Njia moja kwa kuongezeka kwa uwekezaji wa miundombinu, maeneo ya ushirikiano kwa kiuchumi na biashara.

    Walisema kuwa BRI itaendelea kuheshimu uhuru wan chi wanachama na kuongeza kuwa kila nchi itaweka vipaumbele vya maendeleo.

    "Tumekubaliana kwamba tutaendelea kuheshimu uhuru na urithi wa kila mmoja na kuthibitisha kwamba kila nchi ina jukumu la haki na msingi kuelezea mikakati yake ya maendeleo kwa mujibu wa vipaumbelw na sheria zake za kitaifa," rais Xi aeleza.

    Viongozi hao wameahidi kupambana na ubaguzi kwa kiuchumi wakisema kuwa haitawezekana kufikia ukuaji hata uchumi kwa kuzingatia kwamba BRI inafunguliwa kwa wote wanaovutiwa na ushirikiano wa wazi.

    "Tumehitimisha kuwa ni lazima tukubali uchumi wa wazi na soko lisilo na ubaguzi wa kimataifa," asema bwana Xi.

    Rais Xi aliahidi tena kupunguza kwa kiasi kikubwa orodha hasi ya uwekezaji wa kigeni, na kuruhusu makampuni ya kigeni kuchukua hisa nyingi au kuanzisha makampuni yanayomilikiwa kabisa katika sekta zaidi.

    China pia inalenga kuagiza huduma na bidhaa zaidi, na iko tayari kuagiza bidhaa na huduma za kilimo za ushindani kufikia usawa wa biashara.\

    Mkutano huo wa mwisho wa kongamano ya pili ya BRI ulihudhuriwa na marais 38 na mkurugenzi mtendaji wa Fedha Duniani (IMF) Christine Lagarde na mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Gutteres.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako