• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Magazeti ya serikali Tanzania (TSN) yatuzwa na gazeti la China Daily kwa ushirikiano China

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:01:23

    Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN), imepongezwa kwa ushirikiano wake kwa vyombo vya habari vya kimataifa, likiwemo gazeti la China Daily linalochapishwa kila siku nchini China.

    Kwa kutambua mchango huo, uongozi wa China Daily umeizawadia TSN cheti wakati wa ziara ya wahariri na waandishi waandamizi 19 kutoka nchi 18 duniani kwa ziara maalumu ya wiki tatu ya kujifunza na kujionea mapinduzi ya kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa ujumla.

    Katika ziara hiyo, Tanzania ilikuwa nchi pekee kutoka Afrika, ikiwa na mwakilishi wa TSN, Eric Anthony ambaye ni Mhariri Mwandamizi anayeratibu gazeti la HabariLEO Afrika Mashariki linalochapishwa kila siku za Jumanne mahsusi kwa soko la nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

    Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara wa China Daily, Sarah Liu, alikabidhi cheti hicho kwa niaba ya Mhariri Mkuu wa China Daily, Zhou Shuchun.

    China Daily, gazeti lenye mtandao mkubwa wa biashara duniani. liliratibu ziara hiyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumin (UIBE) cha jijini Beijing na Chuo Kikuu cha Taaluma ya Lugha za Kigeni (SISU) cha jijini Shanghai.

    Akikabidhi cheti, Liu alisema China Daily inaona fahari kubwa kufanya kazi na TSN, moja ya kampuni bora za habari barani Afrika. Kama ilivyo kwa China Daily inayomilikiwa na Serikali ya China, TSN pia ni mali ya Serikali ya Tanzania, ikichapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, HabariLeo, HabariLeo Afrika Mashariki na Spoti Leo.

    "Tumefarijika sana kwa uwepo wenu watu wa TSN hapa China. Tunafarijika pia kufanya kazi nanyi kwa karibu na tunatarajia kuendeleza ushirikiano na magazeti ya TSN hasa Daily News na HabariLEO, ndiyo maana tunawakabidhi cheti hiki. Tufikishie salamu TSN na kwa Watanzania kwa ujumla," alisema Liu jijini Beijing.

    China Daily ni moja ya magazeti makubwa duniani, likichapisha karibu nakala 900,000 katika nchi mbalimbali. Aidha, kupitia gazeti lake la mtandaoni linalochapishwa kwa lugha saba za kimataifa, China Daily linajivunia kuwa na wastani wa wasomaji milioni 52 kila siku. Lina mtandao mpana wa kihabari na biashara barani Asia, Marekani, Ulaya na Afrika.

    Mbali ya ofisi za Kanda, ina ofisi nyingine na mitambo ya uchapaji 34 kwa ajili ya magazeti yake katika miji mikubwa duniani yakiwemo ya Brussels (Ubelgiji), London (Uingereza), Paris (Ufaransa) na New York, Marekani.

    "Hatuishii kwenye kuchapa magazeti tu, bali tunawafikia pia mamilioni ya wasomaji kote duniani kupitia magazeti yetu mtandaoni na mitandao mingine ya kijamii," alisema.

    Wanahabari hao kutoka nchi washirika wa mradi wa ujenzi wa miundombinu inayounganisha mabara ambayo inahusisha ujenzi wa barabara, madaraja, mabomba na bandari, mbali ya kufanya ziara katika Jiji la Beijing, walitembelea pia Changsha katika Jimbo la Hunan kujionea mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kasi ya kuondoa umasikini maeneo ya vijijini. Walitembelea pia jiji la Shanghai ambalo ni kitovu cha biashara na uchumi ambako walijionea kasi ya maendeleo katika miundombinu, teknolojia na kadhalika.

    Katika jiji hilo, walitembelea jengo la Shanghai Tower ambalo ni la pili kwa urefu duniani likiwa na ghorofa 118, mitambo ya kuzalisha umeme wa nyuklia katika mji wa Qinshan, kampuni ya ndege ya China Eastern yenye ndege zaidi ya 720 ambalo ni miongoni mwa mashirika kumi bora ya ndege duniani na linashika nafasi ya pili nchini China baada ya Air China.

    Mkuti alikabidhi cheti hicho kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah baada ya kuwasili nchini akitokea Beijing China ambaye ameishukuru China Daily kwa kutambua mchango wa magazeti ya TSN katika ustawi wa taaluma ya habari duniani.

    Aidha, amesema TSN inatarajia kufanya kazi kwa karibu na China Daily kwa kuwa ni watu sahihi wanaopiga hatua kwa katika sekta ya habari, huku wakiendana sambamba na changamoto zinazotokana na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako