• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UDSM na Chuo Kikuu cha Beijing kushirikiana utoaji mafunzo katika sheria

    (GMT+08:00) 2019-06-11 09:04:00

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    UHUSIANO baina ya China na Tanzania unazidi kukua katika sekta mbalimbali hivyo kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo wenye historia ya takribani miaka 55 iliyopita bila kuwa na changamoto mbalimbali.

    Katika mahusiano hayo sekta ya elimu na utafiti Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesaini makubaliano ya ushirikiano na Chuo kikuu cha Beijing nchini China kushirikiana katika masuala ya kisheria .

    Makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kati ya shule ya sheria katika UDSM,na chuo kikuu cha Beijing wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya sheria kwa nchi za Afrika.

    Hafla ya uzinduzi huo uliandaliwa na taasisi ya Confucius iliyopo UDSM na kufuatiwa na kongamano kuhusu mkakati wa ukanda mmoja, njia moja.

    Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mkuu wa idara ya sheria katika shule ya biashara UDSM Dk James Jesse alisema Makubaliano hayo yatawezesha vyu vikuu hivyo (UDMS na chuo kikuu cha Beijing) kuwa na program za kubadilishana wanafunzi wa sheria kutoka china na Tanzania wanaotokea katika vyuo vikuu hivyo.

    Alisema watashirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu mafunzo ya sheria ikiwemo kufanya tafiti za pamoja,program za kubadilishana uzoefu,program fupi na mengineyo.

    Alisema wanafunzi na wahadhiri kutoka shule ya sheria UDSM wataweza kusafiri kwenda chuo kikuu cha Beijing kwa shunguli mbalimbali pamoja na kutoka china kuja Tanzania kwa mafunzo na masuala mengine.

    Akifungua hafla hiyo,Profesa wa shule ya sheria katika UDSM, Bonaventure Rutinwaalisema ushirikiano na kituo cha ushirikiano Afrika katika mafunzo ya sheria kilichozinduliwa Dar es Salaam itaongeza ushirikiano na uhusiano katika kituo hicho.

    Alisema wanafunzi watahamasika kupata uelewa kutoka mifumo mbalimbai ya sheria katika kujifunza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako