• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania kushiriki michuano ya vijana chini ya miaka 11 China

    (GMT+08:00) 2019-06-18 09:29:32

    Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    Tanzania ni kati ya nchi nne Afrika zitakazopeleka timu za vijana walio na umri wa chini ya miaka 11 katika mashindano yatakayofanyika nchini China kuanzia Juni 23 hadi 30 mwaka huu.

    Timu ya vijana wa Tanzania ni kutoka taasisi ya kukuza na kuinua vipaji kwa vijana ya Future stars ya mkoa wa Arusha watakuwa wawakilishi watakaoshiriki michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha timu nane, nne kutoka Afrika na nne kutoka China.

    Mkurugenzi wa "Future stars academy" Alfred Itaeli anasema mashindano hayo yanaandaliwa na chama cha michezo China na kushirikisha vijana ambapo Tanzania ndio watawakilisha kama Future stars huku timu zingine za Afrika ni kutoka Kenya, Ethiopia na Nigeria.

    Anasema mashindano hayo yatachezwa wiki moja na yatafanyika katika mji wa Loudi city katika jimbo la Hunnan nchini China.

    Anaeleza kuwa msafara wa timu hiyo utaondoka Juni 21 mwaka huu wakiwa na wachezaji 16 na viongozi saba.

    "Ni nafasi kwa vijana wetu kujifunza mengi na ni moja ya njia ya kukuza vipaji kutokana na kuwa watacheza na vijana kutoka nchi zingine jambo ambalo litawajengea ujuzi zaidi,"anasema Itaeli.

    Itaeli anasema michuano hiyo ni katika kujenga mahusiano bora katika michezo na itaunganisha jamii na taifa kwani China wanalenga kufika mbali katika soka zaidi ndio maana wamewekeza pia kwa vijana.

    "Future stars tumekuwa tukiendesha mashindano ya chipukizi na tunaamini tutajifunza mambo mengi na tutawaalika nao waje kushiriki michuano yetu na tungefarijika kama tungepata viongozi wakatuaga na kuwapa vijana Bendera ya Taifa,"anasisitiza Itael.

    Miongoni mwa wachezaji watakaoenda kushiriki michuano hiyo Aman Musa alisema wataenda kupambana ili waweze kuendelea kukuza vipaji vyao kwani watakutana na wachezaji kutoka nchi zingine.

    Naye mchezaji Sabeer Rahim alisema atajitahidi kuhakikisha anasaidiana na wenzake kuhakikisha wanaleta ushindi nyumbani.

    Mmoja wa wazazi Samweli Diah anasema anafarijika kuona mtoto wake amepata nafasi ya kwenda China na amekuwa akilelewa katika taasisi ya Future kwa miaka mitano sasa.

    Anasema mtoto wake Joshua Diah amekuwa akifanya vizuri darasani na katika michezo na kusema wachezaji wzuri wananzia katika ngazi za chini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako