• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China, Zanzibar zatiliana saini msaada wa Shilingi Bilioni 33 za Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-06-19 09:59:06

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimetiliana saini ya makubaliano ya msaada wa jumla ya Yuan 100,000,000, sawa na Shiling Bilioni 33 za Tanzania kwa ajili ya kusaidia utekekelezaji wa miradi mbalimbali visiwani humo.

    Fedha hizo, miongoni mwa mambo mengine, zitasaidia katika kufadhili mradi wa nyumba za Watumishi wa Hospitali ya Abdallah Mzee iliyopo Pemba pamoja na ukarabati wa vituo vya Televisheni na Radio za Shirika la Utangazaji Zanzibar, (ZBC).

    Akizungumza katika hafla ya kutiana makubaliano ya ufadhili huo, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Bw, Mohamed Ramia Abdiwawa aliishukuru serikali ya China kwa juhudi zake za kuendelea kuisaidia Zanzibar katika juhudi zake za kuboresha maisha ya wananchi.

    "Zanzibar inashukuru kwa msaada wa China usiokuwa na kikomo," alisema na kusisitiza kuwa Zanzibar imekuwa ikijifunza mambo mengi kutoka China ikiwemo mafanikio kwenye Maendeleo na hivyo itaendelea kuheshimu na kulinda urafiki wao wa muda mrefu na wa kihistoria.

    Aliongeza kuwa China imekuwa ikisaidia kwa kiasi kikubwa sana miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani humo, jambo linaloashiria urafiki wa kweli na wa manufaa.

    "Msaada wa kiuchumi upo katika sura mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya maendeleo ya miundombinu, viwanda na katika nyanja ya kijamii kama vile elimu na afya," alisema Waziri Abdiwawa

    Kwa mujibu wa Waziri huyo, kuanzia miaka ya 2000, China imekuwa ikiipa Zanzibar fedha zinazokadiriwa kufika Yuan 40,000,000 kwa mwaka kama sehemu ya msaada na kuongeza kiasi hicho hadi kufikia Yuan 100,000,000 kuanzia mwaka 2017.

    "Msaada huu umekuwa na mchango mkubwa sana katika sekta za maendeleo na huduma mbalimbali za kijamii," aliongeza Bw. Abdiwawa

    Baadhi ya miradi mikubwa iliyotekelezwa kwa fedha za msaada kutoka kwa serikali ya China ni pamoja na ukarabati wa Uwanja wa Mao Tse Dong, ukarabati wa shule ya sekondari Pangawe na miradi ya visima vya maji Bandamaji kisiwani Unguja.

    Maeneo mengine ni ukarabati wa jengo la ICU cha Hospitali ya Mnazi Mmoja, ukarabati wa Hospitali ya Abdallah Mzee na kufadhili mafunzo ya Watumishi wa umma na wa sekta binafsi wapatao 350 kwa mwaka.

    Kwa upande wake, Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China visiwani Zanzibar Bw Mr Xie Xiao Wu, alisema nchi yake imedhamiria kuhakikisha wanaendelea kuimarisha uhusiano wake na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa manifaa ya pande hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako