• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuibuka kwa teknolojia kutoka China barani Afrika kumekumbatiwa pakubwa

    (GMT+08:00) 2019-06-24 15:37:33

    Na Eric Biegon – NAIROBI

    Uwekezaji wa Wachina katika miundombinu ya teknolojia katika Afrika unaendelea kushika kasi kote barani. Bila ufahamu wa mamilioni ya watumiaji, teknolojia kutoka Beijing sasa inatumika kama uti wa mgongo wa mtandao wa miundombinu katika nchi kadhaa za Afrika.

    Katika hali halisi, fedha kutoka China, teknolojia na ujuzi sasa yana sehemu muhimu katika sekta ya ufundi barani Afrika. Ama kwa kweli, kila aina ya utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa China imejenga sekta ya teknologia Afrika kwa asilimia kubwa.

    Makampuni kama Huawei, ZTE na China Unicom yamesambaza nyaya zao karibu bara lote. Kasi iliyotumika kukamilisha miradi hii pia ni ya ajabu.

    Teknolojia kutoka China unaendelea kujaza mapengo katika njia ambazo huenda zikakosa kuonekana dhahiri kwa haraka. Kwa sasa, mitandao ya kijamii yanatekeleza jukumu muhimu katika maisha ya wenjeji. Wafanyabiashara wanatumia zana hii kujenga bidhaa zao kwa haraka sana. Serikali pia zimetumia rasilimali hii kuboresha utawala na utoaji huduma. Imekuwa jukwaa muhimu katika kujenga mahusiano.

    Lakini kama ilivyo mahusiano kati ya China na Afrika, wakosoaji wanapenda kuangazia pande hasi wa uwepo huu wa teknolojia kutoka China katika Afrika. Zaidi ya hayo, tatizo linaonekana kuwa katika ripoti kuhusu suala hili. Ripoti hasa kutoka mataifa ya magharibi yanaangazia mahusiano haya kama usafirishaji wa matatizo kutoka China kuelekea Afrika badala ya kuangalia matumizi ya chombo hiki kwa serikali za Afrika.

    Makampuni kutoka China yanatumia baadhi ya teknolojia ya ukaguzi na ufuatiliaji ya kisasa ambayo hutumika katika nchi kadhaa. Lakini bado Marekani imekuwa ikitoa onyo kwamba teknolojia zilizotengenezwa na makampuni zinazomilikiwa na Wachina yana hatari za usalama.

    Kwenye kampeni hii, Washington inasema vifaa vinavyotumia mifumo vilivyotengenezwa na China vinaweza kutoa uwezo kwa Beijing kupeleleza serikali za Afrika kwa njia haramu.

    Hata hivyo si Wachina pekee wanaohamisha teknolojia Afrika. Marekani, Israeli, Ufaransa na Italia, kwa mfano, wamekuwa wakifanya hivyo. Kwa miongo kadhaa sasa, makampuni ya teknologia kutoka mataifa ya Magharibi yamekuwa yakihusika sana katika kutoa huduma za kiufundi kwa serikali za Afrika.

    China ni sehemu tu ya wahusika katika soko la kimataifa za nchi zinazaotoa aina hii ya teknolojia. Miradi mingi maizi yanayohusisha fedha kutoka China na makampuni katika nchi za Afrika yanalenga kufanya miji kuwa salama kwa mifumo ya ufuatiliaji.

    Hadi sasa hakuna aliyedhibitisha Afrika kuwa teknologia hii inatumika katika kukandamiza mirengo ya upinzani. Na hapa ndipo palipo na tatizo. Iwapo ni suala la serikali za Afrika kutumia vyombo hivi kuendeleza ukandamizaji, basi si tatizo la China lakini badala yake ni watu au viongozi ambao wanatumia teknolojia hizi kwa ajili ya maslahi yao wenyewe ya kibinafsi.

    Teknolojia kutoka Beijing kulingana na wale wanaochagua kuangalia upande chanya ni sababu kuu ya mabadiliko na maendeleo ambayo ni dhahiri katika miundombinu, kilimo, mawasiliano na sekta ya viwanda.

    Marekani inaendeleza kampeni ya kutaka makampuni ya kitekinologia kutoka China kama Huawei yapigwe marufuku katika nchi nyingi, lakini nchi za Afrika kwa kiasi kikubwa zimepuuza mwito huu.

    Mwishoni wa kongamano la Ukanda Mmoja Njia Moja jijini Beijing mwezi Aprili, kwa mfano, China ilitia saini makubaliano yanayogharimu mabilioni ya pesa ya ushirikiano kati ya Kenya na Huawei kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa kituo cha Data na vifaa maizi za miji.

    Chini ya mpango huu, Huawei itajenga kituo cha taifa cha data ya wingu, mitandao maizi ya ICT, teknologia ya kutoa suluhisho la trafiki, kati ya mambo mengine yatakayorahisisha huduma za biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako