• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jinsi FOCAC inavyoendelea kunufaisha Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-06-26 09:19:46

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    JUKWAA la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) limeendela kunufaisha Tanzania na nchi zingine za bara hilo kwa ujumla.

    Jukwaa hili la ushirikiano kati ya China na Afrika lilianzishwa Oktoba mwaka 2000 wakati wa mkutano wa mawaziri wa Afrika uliofanyika jijini Beijing. Wanachama wake ni China pamoja na mataifa 53 ya Afrika ambayo yana uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika.

    Mwaka 2015, katika mkutano wa Marais wa Afrika na China, nchi hiyo ya Asia ya Mashariki iliahidi kutoa Dola za Kimarekani Bilioni 60 kwa bara la Afrika ambayo ingesaidia katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo. Sehemu ya fedha hizo zilikuwa mikopo ya riba nafuu na misaada isiyi kuwa na masharti yoyote.

    Kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga, kati ya fedha hizo, Dola za Kimarekani Bilioni 10 zilitengwa mahsusi kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali katika nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia na Afrika Kusini.

    Baada ya mkutano huo wa mwaka 2015 uliofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa nchini Tanzania chini ya ufadhili wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.

    Moja ya miradi mikubwa iliyotekelezwa nchi Tanzania ni mkataba ya kisasa ya Chuo Kikuuu cha Dar es Salaam (UDSM) Yenye uwezo wa kuhudumia wasomaji 2,100 kwa wakati mmoja.

    Maktaba hiyo ya kisasa kuliko zote katika nchi za Afrika chini ya Jangwa la Sahara imejengwa kwa msaada wa Serikali ya China wa shilingi bilioni 90 ikiwa na uwezo wa kubeba makasha 400,000 ya kuhifadhia vitabu papmoja na kumbi za mikutano zenye uwezo wa kubeba watu 600.

    Kati ya Jumatatu na Jumanne, Juni 24 na 25 mwezi Juni, Mkutano wa Mawaziri wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika umefanyika jijini Beijing ili kutathmini utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa Marais wa Jukwaa hilo mwaka jana, 2018.

    Katika mkutano huo wa mwaka jana, China kupitia kwa Rais wake Xi Jinping alitangaza tena kutoa fedha takribani Dola za Kimarekani Bilioni 60 kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya Maendeleo barani humo.

    Kwenye mkutano huo, Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof Palamagamba Kabudi.

    Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Balozi wa China nchini Tanzania Bi. Wang Ke aliishauri nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki kutumia vizuri Mkutano huo kuimarisha ushirikano wake na nchi hiyo ya Asia ya Mashariki.

    Ikiwa ni ishara ya Tanzania kuendelea kunufaika na jukwaa hili, Tanzania kwa mara nyingine tena imetia saini Mkataba wa kupatiwa fedha za msaada wa Shilingi Bilioni 60 za Tanzania kutoka Serikali ya Watu wa China bila ya masharti yeyote ambapo Serikali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki itaamua matumizi yake katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake.

    Hii ni hatua nyingine inayotoa fursa kwa Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo hasa kwa nyakati hizi ambazo nchi hiyo iko katika harakati za kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

    Vilevile, Tanzania imeendelea kunufaika na jukwaa hilo kwani nchi hiyo ya pili kwa utajiri duniani imekubali kutoa fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya upanuzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ili kuwa Taasisi Mahiri ya Tiba ya Moyo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

    Ni dhahiri pia kwamba mazungumzo yaliyofanywa kati ya wawakilishi wa mataifa hayo mawili yalilenga kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya China na Tanzania sambamba na kuibua maeneo ya kipaumbele na kimkakati yatakayotekelezwa kwa ushirikiano baina ya China na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako