• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawapatia wanawake wa mikoa sita Tanzania vyerehani 330 na kutoa vifaa 380 kwa watu wenye ulemavu

    (GMT+08:00) 2019-07-01 09:39:34

    Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    CHINA imetoa msaada wa vyerehani 330 kwa vikundi vya wanawake katika mikoa sita na vifaa 380 vya watu wenye ulemavu vyote vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 51,617 (takribani Sh milioni 121.3).

    Mikoa itakayonufaika na msaada huo ni vikundi vya wanawake kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Dar es Salaam, Dodoma, Simiyu na Tabora. Vifaa vya watu wenye ulemavu vina thamani ya Dola za Marekani 15,000.

    Balozi wa China nchini, Wang Ke akikabidhi vifaa hivyo alisema misaada hiyo inatolewa chini ya Programu ya RAFIKI yenye lengo la kuwainua wanawake na kuwasaidia kukabiliana na changamoto kwa watu wenye ulemavu.

    Anasema kwa mwaka huu kupitia programu ya Rafiki, China imetoa vyerehani 330 ambapo kati ya hivyo, 180 vinatumia umeme vikiwa na thamani ya fedha ya China Yuan 800 kila kimoja na vyerehani 150 ni vya kawaida ambapo kila kimoja thamani yake ni Yuan 700.

    "Kuna usemi usemao ukimuelimisha mwanaume utakuwa umemwelimisha mtu mmoja lakini ukimuinua mwanamke utakuwa umeisaidia familia nzima. Sisi tumeona tuwasaidie wanawake wa mikoa sita vyerehani, tunajua kwa kufanya hivyo wataweza kuinuka kiuchumi, kuhudumia familia zao na kulipa ada za watoto alisema

    Ke anabainisha kuwa kwa muda mrefu China imekuwa ikishirikiana na Serikali ya Tanzania katika sekta ya afya na elimu kwa kutoa fursa za masomo kila mwaka lakini sasa kupitia programu hiyo imeamua kusaidia makundi yenye mahitaji zaidi.

    Balozi anasema katika kuendeleza ushirikiano huo, China inashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuboresha Chuo cha Usafirishaji (NIT) ili kuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji na pia kuboresha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

    Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alishukuru Serikali ya China, na kuwataka wanufaika wa msaada huo kuutumia ipasavyo.

    "Mmepewa msaada huu mkautumie vizuri, haitakuwa jambo jema kama tutakuta vyerehani hivi vinauzwa mitaani, tunaka viwafikie walengwa na wanaufaike navyo," anasema.

    Anabainisha kuwa anzania inakadiriwa kuwa na watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa takribani watu milioni 2.5 ambao kama watawezeshwa watakuwa na manufaa makubwa kwa taifa.

    Naye,mkurugenzi wa Taasisi ya Chief Promotions, Amon Mkoga anasema msaada huo utasaidia wanawake wajane wa Mkoa wa Tabora kupata fedha za kuendesha maisha yao na kulipia kadi za bima ya afya kwao na watoto wao.

    Hafla hiyo pia lihudhuriwa na Naibu Waziri anayeshughulikia walemavu, Stella Ikupa na Waziri wa Uwekezaji Angela Kairuki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako