• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuunga mkono Afrika katika maendeleo: Bwana Lu Kang

    (GMT+08:00) 2019-07-10 08:37:43

    NA VICTOR ONYANGO

    China itaendelea kuunga mkono Afrika kufikia ndoto yake ya viwanda, Lu Kang, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje alisema.

    Akizungumza Jumanne alipokutana na waandishi wa habari zaidi ya 70 kutoka Afrika, Asia na Pasifiki na nchi za Kilatini, bwana Lu aliwahimiza nchi za Kiafrika kuja na njia yao ya maendeleo ambayo inafaa masharti yao yasiyo na ushawishi wa nje.

    "Kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita, China imekutana na changamoto nyingi ndani na nje hata sasa, suala la msuguano wa biashara. Licha ya yote haya, China ilikuja na njia yake ya maendeleo na hiyo ndiyo imeendelea kusaidia China kufanikiwa katika suala la maendeleo na ndio nini marafiki zetu Afrika wanapaswa kufanya, " asema bwana Lu.

    Aliongeza kuwa China inashirikiana na Afrika daima itategemea mashauriano makubwa bila ya masharti ya kisiasa na hali ya kuweka.

    Bwana Lu alisema kuwa Rais Xi Jinping amekuwa akisisitiza juu ya haja ya kugawana knowledgehow ya teknolojia ya China na Afrika na ambayo itafanyika na sio Afrika peke yake bali pia nchi nyingine zinazohitaji.

    Aliwahimiza waandishi wa habari kuchukua nafasi waliyo nayo nchini China sasa ili kuhakikisha kwamba wanajifunza njia za kijamii na kiuchumi za China na kushirikiana na nchi zao ili kukuza ukuaji wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako