• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania na China kushirikiana kuendeleza utamaduni wa nchi hizo

    (GMT+08:00) 2019-07-12 08:45:09

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    SERIKALI ya Tanzania imehaidi itaendelea kutambua mchango wa China na kushirikiana nao katika kukuza utamaduni na sanaa nchini.

    Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo,Nicolas William alisema hayo wakati wa ufunguzi wa wiki ya utamaduni wa muziki wa jadi wa kundi la Mongolia kutoka China lililofanyika jijini Dar es Salaam.

    Alisema kuna mambo mengi yanayofanywa na serikali ya China kupitia ubalozi wake katika muda mfupi tangu Tanzania iliposaini mkataba wa makubaliano katika kushirikiana kwenye masuala ya utamduni mwaka 2013.

    Alisema kuna mambo machache kama kutoa nafasi za mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa serikali kusoma kozi za sekta ya sanaa na utamaduni pamoja na lugha ya kichina na menfine yanayofanyika chini ya ufadhili wa serikali ya China.

    Alihaidi Tanzania kuendelea kutimiza wajibu wake kwa kushirikiana na ubalozi wa China kuhakikisha sekta ya utamaduni na sanaa zinakuwa chanzo kikuu cha kudumisha ushirikiano huo.

    "Tanzania tunajivunia kwa kuwa a utajiri wa rasilimali za Kiutamaduni ambazo si rahisi kuzipata katika nchi nyingine duniani"alisema

    Alitoa mfano kuwa Tanzania kuna makab ila zaidi ya 120 na yote yana utamaduni wake hivyo ni fursa ya China hususan vikundi kama hivyo vya utamaduni vinapokuja nchini kuzungumza na vikundi vingine vya sanaa na Uatamaduni ili kubadilishana uzoefu na kuzitumia fursa zilizopokwa pande zote mbili.

    Mshauri mwelekezi wa Masuala ya Utamaduni China, Gao Wei alisema katika wiki hiyo ya utamaduni wa muziki wa jadi wa watu wa China inasaidia kuimarisha ushoirikiano na mahusiano ya kiutamaduni baina ya nchi hizo.

    Katika wiki hii, kumekuwa na nyimbo za kiutamaduni pamoja na michezo, maonesho ya kazi za mikono na picha ambapo raia wa China zaidi ya 200 wako katika vituo mbalimbali 34 kikiwemo hiki cha Tanzania kusherehekea wiki hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako