• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi wa kidato cha nne katika sekondari 16 Tanzania kufanya mtihani wa taifa wa somo la lugha ya kichina mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-07-15 09:46:39

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    KATIKA kuhaikikisha Tanzania inakuwa na wataalamu katika lugha ya kichina kwa wananchi wake kwa mara ya kwanza mwaka huu, wanafunzi wa shule 16 za Sekondari nchini wanatarajia kulifanyia mtihani wa taifa wa kidato cha nne wa somo hilo baada ya kufundisha miaka

    Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inakusudia kukiteua Chuo cha Ualimu cha Marangu kilichopo mkoani Kilimanjaro kufundisha kozi la lugha ya kichina kwa walimu tarajali ili baadaye waweze kufundisha somo hilo katika shule mbalimbali za Sekondari za Serikali nchini.

    Naibu Katibu mkuu wa wizara hiyo anayesimamia Elimu, Dk Ave Maria Semakafu amesema hayo mjini hivi karibuni katika akifungua kituo cha darasa la ya lugha ya kichina katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kupitia Taasisi ya Confucius ya China.

    "Kwa sasa wizara inafanya mazungumzo ya kuingia mkataba na Taasisi ya Lugha na Utamaduni wa Kichina makao makuu ili tuanzishe walimu wa lugha ya kichina katika Chuo chetu cha Ualimu kilichopo Marangu , liwe ni somo kama ilivyo kwa lugha ya Kiingereza na Kiswahii" amesema Dk Semakafu.

    Naibu Katibu mkuu amesema, wizara imeweza kuanzisha masomo ya lugha ya kichina kama somo la kufanyia mtihani na kwa mwaka huu 2019, ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa shule 16 za Sekondari watalifanyia mtihani wa kidato cha nne na hayo ni mafanikio makubwa.

    Dk Semakafu anasema, mpango wa kufundisha lugha ya kichina katika shule 16 za sekondari nchini za Serikali ulianza rasmi Januari mwaka 2016.

    Anasema wizara ilichukua walimu kwa baadhi ya shule za Sekondari pamoja na kutoka Taasisi ya Elimu walienda China kwa miezi 10 na waliporudi wameleta kitu kizuri kwenye somo la lugha ya kichina na mafanikio haya yamesukuma kuanisha katika moja ya vyuo vyetu vya Ualimu (Marangu) mafunzo ya ualimu wa lugha ya kichina.

    Dk Semakafu pia alibainisha kuwa Taasisi ya Confucius ya China hapa nchini kwa kuandisha na kufundisha lugha ya kichina katika Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Waislamu ch Morogoro (MUM) ambapo Chuo Kikuu cha Waislamu kimeonesha mafanikio makubwa hadi kuweza kuanzishiwa Kituo rasmi.

    Naye Katibu wa Idara ya Taasisi ya Lugha na Utamaduni wa Kichina katika Ubalozi wa China hapa nchini, Zhang Bing anasema, Tanzania na China ni marafiki wa muda mrefu ulianzishwa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Mwasisi wa Taifa la China, Mao Zedong.

    Anasema, Taasisi ya Confucius ya China ipo kwenye vyuo vikuu vitatu nchini Tanzania na kuiwezesha nchi yake kuleta walimu 130 kutoka nchini mwao kwa ajili ya kufundisha na wapo wanafunzi wa Tanzania wanaojifunza kichina zaidi ya 17,000.

    Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Balozi Profesa Abilahi Omar anasema, Chuo kimeendelea kupata mafanikio katika nyanja mbalimbali za kielimu ikiwemo na ongezeko la udahili wa wanafunzi wa shahada zinazotolewa Chuoni hapo wakiwemo wa somo la lugha ya kichina ambapo wengi wao wamefanikiwa kupata ufadhili wa kwenda kujiendeleza katika vyuo vikuu vya nchini China kwa ngazi za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako