• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya Utalii China inavyobebwa na Wachina Wenyewe

    (GMT+08:00) 2019-07-16 09:47:24

    Na Theopista Nsanzugwanko

    UTALII nchini China ni sekta muhimu kwa maendeleo ,unaochangiwa na raia wenyewe wa nchi hiyo kutokana na kuwa na vivutio vya kila aina ikiwemo maeneo ya historia mbalimbali kuanzia dini,siasa,maendeleo ukuaji wa miji na mengineo imekuwa vivutio katika miji mbalimbali nchini humo huku idadi kubwa ya watalii wakiwa ni kutoka ndani ya nchi hiyo tofauti na nchi nyingine.

    inaelezwa kuwa nchini humo kuna miji zaidi ya 100 ambayo ina utalii bora wa aina mbalimbali baadhi yake ni Shanghai, Beijing, Tianjin, Chongqing, Shenzhen, Hangzhou, Dalian, Nanjing, Xiamen, Guangzhou, Chengdu, Shenyang, Qingdao, Ningbo, Xian, Haerbin, Jinan, Changchun na Lasha huku kukiwa na miji kadhaa ambayo ni maarufu kwa utamaduni kwani nchi hiyo imekuwa na tamaduni mbalimbali ambazo zimeenziwa na kuendelezwa kizazi hadi kizazi huku wakijivunia mnyama aina ya 'Panda' anayepatikana nchini humo.

    Ukifika katika nchi hiyo, Kwa safari ya kikazi kibiashara au vinginevyo ni lazima utapelekwa katika maeneo yao ya utalii ili kuwa balozi wake na kutangaza nchini mwake hususan katika maeneo maalufu kama Great Wall ,Forbidden City iliyopo beijing ambapo watu wengi kutoka maaneo mbalimbali wamekuwa wakihakikisha wanafika juu kabisa.

    Mbali na utalii katika maeneo hayo pia kuna Tibet, Shanghai, Gobi, Yangtze au Yellow River, yamekuwa maarufu hata kwa wanafunzi na vijana huku China ikiwa kitovu cha shughuli za biashara imefanya watu kutoka maeneo mbalimbali duniani kutembelea nchi hiyo.

    China imekuwa ikiuza bidhaa mbalimbali popote duniani ,pamoja na kuingiza bidhaa hivyo kuwa rahisi kwa wananchi wa maeneo mbalimbali kupata kile anachohitaji hata kutoka nchi kubwa duniani,pia wamekuwa wakishuhudia bidhaa za uchongaji pamoja na utalii wa vyakula vya aina mbalimbali kutoka China na maeneo mengine.

    Ukiwa China, katika shughuli mbalimbali, lazima utafanya utalii kwa kushuhudia makabila mbalimbali ya nchi hiyo na tamaduni zake kutoka maeneo mbalimbali kukiwa na lugha,mavazi na tamaduni nyingine ambazo zimetambuliwa na UNESCO kama urithi wa dunia.

    Takwimu za utalii zilizotolewa mwezi Mei mwaka huu zinaonesha kuwa watalii walioingia nchini ni milioni 143 na kuingiza Dola za marekani bilioni 129.6 huku safari za nje zikiingiza dola milioni 166 na watalii wa ndani trilioni 6.06 walioingiza mapato ya CNY Trilioni 5.6 ambapo kwa ujumla waliingiza mapato ya CNY Trilion 6.52.

    Wapo wanaoweza kushangaa kwa jinsi watalii wa ndani walivyokamata sekta hiyo,lakini uzalendo kwa wananchi unafanya kila sehemu ya utalii unapotembelea raia wa nchi hiyo wakiwa wengi kuliko nchi nyingine kwa wanaotoka sehemu moja ya nchi kwenda kwenye sehemu nyingine kwa kutenga fungu maalum kuhakikisha wanatembelea vivutio vingi vya utalii.

    ili kuhakikisha utamaduni huo unaendelea,watoto pamoja na wanafunzi mashuleni wamekuwa na ziara za utalii maeneo mbalimbali ,hata kwa maeneo ambayo uwezo wa kifedha ni mdogo wamekuwa wakitembelea vivutio vya maeneo yao.

    Sekta ya utalii ni muhimu na idadi yao imekuwa ikiongezeka kila mwaka ,tangu kuanza kwa sera ya kufungua milango mwaka 1978 mpaka sasa na kuna mawakala wa usafiri kwa ajili kusafirisha wageni 1349 kati yao 248 wakiwa Beijing, Shanghai, Tianjin na Chongqing hivyo kuwa rahisi kufika China na kufanya safari za kutembelea maeneo mbalimbali .

    Mwaka jana, watalii toka nje walifikia million 141.2 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1.2 ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia huku maeneo 10 yaliyotembelewa na watalii wa nje yakiwa Shanghai, Beijing, Guangzhou, Chengdu, Chongqing, Nanjing, Kunming, Wuhan, Xi'an na Hangzhou huku asilimia 82 ya wasafiri wa chini walitembelea Beijing katika maeneo maarufu ya The forbidden city na The great wall of China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako