• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Beijing Construction Engineering Group yakanusha ujenzi chini ya viwango

    (GMT+08:00) 2019-07-17 08:59:05

    Na Majaliwa Christopher

    KAMPUNI ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China imekanusha madai kuwa kazi ya ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar haukukididhi viwango vya kimataifa.

    Hivi karibuni, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar walionyesha kutoridhishwa na namna ambayo jengo la uwanja huo ulijengwa wakidai kuwa ulikuwa chini ya viwango, madai ambayo yalikanushwa na kampuni ya BCEG ambayo ilitekeleza mradi huo.

    "Ujenzi wa jengo jipya la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ulijengwa kwa mujibu wa viwango viliyoanishwa katika mkataba wetu na ulikidhi viwango vya kimataifa," kampuni hiyo ya China ilisema jana, Julai 16 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

    Taarifa hiyo iliongeza kuwa baada ya kumalizika kwa mradi huo, ukaguzi kuthibitisha ubora na viwango ulifanywa na Serikali na hatimaye kupewa cheti cha makabidhiano.

    "Michoro ya ujenzi, mashine na vifaa vyote vilivyotumika kwenye mradi huu zilisimamiwa na kuthibitishwa na mkandarasi pamoja na mwajiri," taarifa hiyo ilisema na kuongeza kuwa, taratibu zote hizo zilifatwa kwa mujibu wa makubaliano yaliyokwepo kwenye mkataba wa utekelezaji wa maradi huo.

    Kampuni hiyo imeonya kuwa itachukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote ambaye kwa makusudi hujihusisha na tabia za kuichafua kwenye vyombo vya habari na kwa jamii kwa ujumla.

    Imesisitiza kuwa itaendelea kutekeleza miradi yote inayoshinda nchini Tanzania na maeneo mengine kwa kufata vigezo vyote vilivyoko kwenye mikataba ambayo kimsingi hukidhi viwango vya kimataifa.

    "Kampuni ya BCEG itaendelea kutekeleza miradi yote inayoshinda nchini Tanzania kwa ufanisi. Huu ndo msingi wa ushirikiano katika ya Tanzania na China," taarifa hiyo iliongeza.

    Jengo hilo jipya lina mlango mkubwa (Main Entrance) kwa ajili ya kuhudumia abiria wote wa kimataifa na kitaifa na lina uwezo wa kuwahudumia abiria wapatao 500 kwa wakati mmoja.

    Taarifa ya Beijing Construction Engeering Group inakuja siku chache baada ya kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE), East Africa Limited inayotekeleza miradi mbalimbali nchini Tanzania kukanusha madai kuwa kazi zake zimekuwa zikitekelezwa chini ya viwango.

    Kampuni hiyo ya CRJE ilisema miradi yote inayotekeleza ni kwa mujibu wa makubaliano na viwango vilivyowekwa.

    Baadhi ya miradi iliyowahi kutekelezwa na CRJE Zanzibar ni pamoja na hoteli ya nyota tano ya Kiwengwa iliyokamilishwa mwaka 2005 hoteli ya Kizimkazi iliyokamilika mwaka 2011, hoteli ya Park-Hyatt pamoja na miradi mingine ya serikali ikiwemo jengo la Bodi ya Mapato Zanzibar

    Kampuni hiyo ya ujenzi kutoka China ilitoa taarifa hiyo siku chache baada ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi --Zanzibar kudai kuwa makampuni ya nje ya ujenzi yanayotekeleza miradi mbalimbali visiwani humo yamekuwa yakifanya kazi chini ya viwango vya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako