• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara 25, kutoka Kampuni 15 za Jimbo la Zhejiang China kufanya ziara ya siku tatu kusaka fursa za biashara Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-07-22 10:30:25

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    UWEKEZAJI wa China kwa anzania mwaka jana umefikia dola za Marekani Bilioni saba na kufanya nchi hiyo kuendelea kuongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwa na kampuni 200 zilizowekeza na kutoa huduma nchini hadi sasa,ambazo wawakilishi wake walipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo.

    Huku mikataba mpya ambayo serikali imesaini na China mwaka jana imefikia Dola za Marekani bilioni 1.3 katika miradi ya miundombinu, madini, kilimo na Viwanda, hoteli, nyumba na sekta ya fedha.

    Katika kuendeleza uwekezaji baina ya nchi hizo mbili ,wafanyabiashara 25, kutoka Kampuni 15 za Jimbo la Zhejiang China, utafanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania kusaka fursa za biashara,ziara hiyo itafanyika kati ya Julai 20 hadi 23, mwaka huu na utafanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

    Taarifa ya kitengo cha Mawasiliano cha Serikali cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilisema kuwa ujumbe huo utaongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Jimbo hilo, GE Huijun.

    Taarifa hiyo ilisema lengo la ziara hiyo ni kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini na inalenga kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Jimbo la Zhejiang na Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile teknolojia, mawasiliano, ujenzi na uchukuzi, afya na madini.

    Tayari China na Tanzania zina mahusiano ya muda mrefu zaidi ya miaka 45 ambapo bidhaa mbalimbali zinaingizwa nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na vyakula, magari, nguo, bidhaa za viwandani, vipuri vya magari na mitambo, vifaa vya umeme na vile vya chuma wakati Tanzania inauza kwenda China vyakula vya baharini, ngozi mbichi, magogo, shaba, Mihogo na vifaa vya mbao.

    Mwenyekiti huyo wa jimbo la Zhejiang, GE Huijun pia atafuatana na viongozi 13 wa Serikali ya Zhejiang kwenye ziara hiyo ambayo itaanzia Zanzibar leo.

    Ukiwa Zanzibar, ujumbe huo utatembelea maeneo ya viwanda ya Amani na Fumba kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji. Aidha, ujumbe huo utakutana na Mamlaka ya Uwekezaji na Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Zanzibar kwa madhumuni ya kuanzisha ushirikiano.

    Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa ujumbe huo utashiriki ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara kutoka jimbo la Zhejiang utakaofanyika jijini Dar es Salaam Julai 22, mwaka huu na kufikia tamati ya ziara yao Julai 23, mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako