• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi mdogo wa China Zanzibar asema Misaada ya China Zanzibar inalenga kuimarisha uchumi na huduma za jamii kwa wananchi

    (GMT+08:00) 2019-07-29 10:08:15

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China imesema misaada yake inayotoa inalenga katika kuimarisha uchumi na huduma za jamii kwa wananchi wa Zanzibar.

    Hayo yalisemwa na Balozi mdogo wa China aliopo Zanzibar Xie Xiaowu wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Verder iliopo Mtoni Unguja.

    Anasema uhusiano wa China na Zanzibar ulianza mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964 ikiwa nchi hiyo miongoni mwa nchi za mwanzo kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar na kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda.

    Balozi Xiaowu anasema mahusiano hayo yamekuwa yakiendelea katika nyanja mbalimbali ikiwemo China kuleta madaktari bingwa kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwa wananchi wa Zanzibar.

    Anatoa mfano wa ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee iliyopo Mkoani Pemba ni mfano wa ushirikiano wa nchi hizo katika sekta ya afya.

    Anasema kwa miaka 55 sasa China imekuwa ikileta madaktari bingwa Zanzibar na kutoa matibabu ya aina mbalimbali na hii ni awamu ya 29 ya timu ya madaktari 740 kutoa huduma za kiafya nchini.

    Alitoa mfano wa timu ya madaktari hao imeweza kuwatibu zaidi ya wagonjwa milioni saba huku wakifanya upasuaji kwa wagonjwa 200,000 pamoja na kuokowa maisha ya wagonjwa 40,000 waliokuwa katika hali mbaya za kiafya.

    "Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ukiwemo mradi wa kupambana na ugonjwa wa kichocho ambao ni hatari kwa afya za watoto pamoja na wanafunzi wa shule," alisema.

    Aidha Balozi Xiaowu anasema matarajio yake makubwa kwamba msaada wa jumla ya Sh Bilioni 34 zilizotolewa na nchi hiyo utatumika vizuri kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za madaktari bingwa katika hospitali ya Abdalla Mzee na uimarishaji wa mitambo ya kurushia matangazo ya vyombo vya habari vya SMZ.

    "Serikali ya Jamhuri ya watu wa China tumetoa msaada jumla ya Sh Bilioni 32 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi katika hospitali ya kisasa ya Abdalla Mzee, Pemba...msaada huo pia utatumika kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano ya mitambo vya shirika la utangazaji la Zanzibar ZBC," anasema.

    Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar Dk Juma Mohamed anasema Zanzibar inathamini misaada inayotolewa na China ambayo imekuwa kichocheo cha kukuza uchumi na mawasiliano.

    Alisema Zanzibar ni miongoni mwa nchi ambazo zinafaidika kwa kiasi kikubwa na misaada inayotolewa na Jamhuri ya Watu wa China ambayo imeanza tangu mwaka 1964 mara baada ya mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako