• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yawezesha Tanzania kuwa ya kwanza Afrika Mashariki kutibu moyo unaokwenda mbio kwa kuipatia mashine yenye thamani ya Shilingi milioni 500

    (GMT+08:00) 2019-07-29 10:08:55

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    CHINA imewezesha Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kutibu wagonjwa wa moyo ambao unakwenda mbio baada ya mfumo wa umeme wa moyo kuharibika, tatizo ambalo wagonjwa walikua wakipelekwa nje kupata matibabu .

    Serikali ya China imetoa msaada wa mashine ya kutibu tatizo hilo lijulikanalo kitaalamu kama SBT kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), mashine hiyo ina thamani ya Shilingi milioni 500.

    Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohammed Janabi amesema kabla hawajapata kifaa hicho wagonjwa hao walikuwa wakipelekwa nje ya nchi kwa matibabu ambapo madaktari wanaingia kifaa ndani ya moyo na kuunguza sehemu ambazo zinasababisha hali hiyo kwa mgonjwa na mpaka sasa wagonjwa watatu wameshafanyiwa matibabu hayo.

    "Kifaa ambacho kimetolewa kwetu kitatusaidia kutibu wagonjwa ambao mfumo wa moyo umeharibika na mapigo ya moyo yanaenda mbio, kabla hatujapata mashine hii wagonjwa tuliwapeleka nje ya nchi," anasema Profesa Janabi.

    Anasema moyo una mfumo wa umeme ambao hupata matatizo tofauti na tatizo hilo ni moja ya matatizo yanayohusisha mfumo wa umeme na kuongeza kuwa athari ya tatizo hilo ni kupata kiharusi.

    Profesa Janabi anasema wataalamu wa JKCI wanaendelea kupatiwa mafunzo ya kutumia mashine hiyo na madaktari wengine kutoka Marekani wanatarajiwa kufika nchini mwishoni mwa wiki hii na watu kati ya 20 na 30 watapatiwa matibabu hayo katika kipindi cha wiki mbili.

    Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu anasema ni mara ya kwanza kwa EAC kuwa na mashine ya namna hiyo na kupongeza ushirikiano baina ya Tanzania na China.

    "Kwa mara ya kwanza Tanzania tunakuwa na mashine hii ambayo haipo katika nchi zote za Afrika Mashariki, Agosti mwaka jana nilikwenda China na tuliingia makubaliano na serikali ya China kushirikiana kati ya wizara zetu leo hii makubaliano hayakuishia kwenye makaratasi," anasema Waziri huyo.

    Anasema China ni kati ya nchi ambazo zimeisaidia JKCI kufikia matibabu ya kiwango cha juu wakati awali wagonjwa walikuwa wakipelekwa nje ya nchi lakini sasa wanatibiwa nchini.

    Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI, Profesa William Mahalu anasema taasisi hiyo ilikuwa na ndoto aliyokuwa nayo miaka mingi na kwamba alitamani siku moja Tanzania ifanye matibabu ya moyo jambo ambalo linafanyika sasa hivyo kutimiza ndoto yake ya mwaka 1978 kufanyika upasuaji wa moyo nchini.

    Aidha anasema bado taasisi hiyo inahitaji teknolojia zaidi ili kuendana na wakati na pia mafunzo kwa madaktari wao ili miaka ijayo kambi za madaktari nchini wafike wachache kwa kuwa JKCI kutakuwa na madaktari wa kutosha na ujuzi wa hali ya juu.

    Naibu Waziri wa Afya wa China, Lin Bin aliahidi kuendelea kusaidia Tanzania katika sekta ya afya kwa kuleta wataalamu, kutoa mafunzo kwa madaktari pamoja na msaada wa vifaa ili kuboresha huduma za afya hapa nchini.

    "Tutaendelea pia kuisaidia JKCI ili iwe kituo cha heshima katika matibabu ya moyo Afrika Mashariki,kwani China na Tanzania zina ushirikiano wa muda mrefu hasa katika masuala ya afya," alisema.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako