• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ufadhili wa China kusaidia Tanzania kupunguza malaria

    (GMT+08:00) 2019-07-29 10:52:27

    Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    TANZANIA imezindua Programu ya Kupambana na Malaria awamu ya pili inayofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na kutekelezwa na Taasisi ya Afya Ifakara, Shirika la Afya Duniani na Chuo Kikuu cha Harvad.

    Akizindua progamu hiyo katika wilaya za Rufiji na Kibiti Mkoani Pwani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Tanzania, Bi. Ummy Mwalimu, alisema kuwa nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki imejipanga kupunguza malaria kutoka asilimia 7.3 hadi kufikia asilimia moja mwaka, 2020.

    Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayopambana kuhakikisha yanautokomeza kabisa ugonjwa wa malaria. Tanzania ilizindua taarifa ya utafiti wa viashiria vya malaria ya mwaka 2017/18, iliyooonyesha kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo kupunguwa kwa asilimia 7.3 ikilinganishwa na matokeo ya tafiti ya mwaka 2015.

    Tathmini hiyo iliiwezesha Tanzania kufuatilia utekelezaji wa mpango wa kupambana na ugonjwa wa malaria ili kufikia azma ya kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

    Jana, Alhamisi, Julai 25, 2019, Bi. Mwalimu alisema tayari wizara imeshaweka mikakati mbalimbali ya namna ya kutekeleza programu hiyo itakayo hakikisha kuwa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria vinapunguzwa kwa kiasi kikubwa.

    "Serikali yetu inafanya kazi kwa nguvu zote kuhakikisha vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria vinapungua. Tumejipanga kufanikisha hili kwa kuongeza bajeti ya wizara pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali," alisema Bi. Mwalimu.

    Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya Wa China, Bw. Li Bin, alisema kuwa nchi yake imefanikiwa kudhibiti kabisa vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria ambao kabla ya hapo ulikuwa ukiangamiza maisha ya mamilioni ya Wachina.

    "Nchi hizi mbili, Tanzania na China, zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu katika sekta mbalimbali kwa karne nyingi zilizopita. Sekta ya afya ni moja ya maeneo tumekuwa tukishirikiana. Nchi yetu imedhamiria Kushirikiana na Tanzania kutokomeza malaria kama tulivyofanya sisi," alisema Bw. Li.

    Nchini Tanzania, kwa mujibu wa taarifa ya 2017/2018, ugonjwa wa malaria ni kati ya maradhi yanayo sababisha vifo vingi nchini humo, ambapo kwa mujibu wa takwimu za kipindi hicho, katika kila wagonjwa 1,000 wa malaria, 9 kati yao hufariki dunia na makundi ya jamii yaliyo katika athari kubwa ya malaria ni watoto na wajawazito.

    Kwa mujibu wa data za Shirika la Afya Duniabni malaria unaua mtoto mmoja kila baada ya dakika mbili huku visa vipya zaidi ya milioni 200 vikiripotiwa kila mwaka.

    Ripoti mpya ya WHO kuhusiana na hali ya malaria duniani --iliyotolewa mwaka 2018-- inaashiria kuwa viwango vya maambukizi havijashuka kati ya 2015 mwaka 2017.

    Afrika inakadiriwa kubeba sehemu kubwa yagharama ya watu walioathiriwa na malaria duniani -mwaka 2017, bara hilo liliripoti 92% ya visa vya malaria na 93% ya vifo vilivyotokana na ugonjwa huo.

    Inakadiriwa kuwa karibu Dola Bilioni 3.1 za Marekani zilitumika kudhibiti na kuangamiza malaria mwaka 2017.

    Mbali na nchi hiyo ya Asia ya Mashariki kusaidia vita dhidi ya malaria nchini Tanzani, pia inatoa mchango katika maeneo mengine ya afya katika taifa hilo la Afrika ya Mashariki .

    Mwaka jana, 2018, China na Tanzania kupitia mawaziri wa afya wa nchi hizo mbili, jijini Beijing, ziliisaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano kati ya wizara zao katika sekta ya Afya.

    Makubaliano hayo yalijumuisha ushirikiano katika tiba, utafiti na mafunzo ya wataalam wa tiba katika fani za moyo, saratani na mishipa na Ubongo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako