• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya CHICO kutoka China yasaini mkataba ujenzi barabara Tanga-Pangani

    (GMT+08:00) 2019-08-05 08:55:05

    Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    KAMPUNI ya China Henan International Company Limited (CHICO) imesaini mkataba wa ujenzi sehemu ya barabara ya Tanga- Pangani yenye urefu wa kilometa 50.

    Utiaji saini mkataba wa ujenzi huo lililofanyika katika viwanja vya Bomani Pangani mjini kati ya Wakala wa Barabara (Tanroads) kwa niaba ya Serikali na Mkandarasi Wang Xiang Gang kwa niaba ya kampuni ya CHICO utokana na mkataba huo sehemu hiyo ya ujenzi wa barabara utagharimu shilingi bilioni 66.8 fedha kutoka serikali ya Tanzania.

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwele alitaka wananchi wa maeneo hayo kutumia fursa za ajira kuwa licha ya barabara kujengwa ili kuwezesha na kurahisisha usafirishaji pia ni fursa za fursa za ajira kutokana na eneo hilo kuwa na utalii wa baharini na kujipatia ajira katika shughuli za ujenzi.

    "Ndugu zangu wana Pangani hii ni fursa kwenu ya ajira na kujiimarisha kiuchumi katika huu mradi wa ujenzi wa barabara....vijana mtapatapa ajira,wakinamama mtauza vyakula, wenye hoteli mtapata wageni wengi msiiachie nafasi hii" alisema.

    Aliongeza" mbali na barabara hiiyo alitangazia tena neema ya mradi mwingine wa ujenzi wa daraja litakalokatiza katika mto Pangani kuelekea upande wa pili lenye urefu wa mita 525 na barabara unganishi yenye urefu wa kilometa 120 hadi Makunge hii ni fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nayo mradi huu utaanza hivi karibuni".

    Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye ni Naibu Waziri wa Maji alisema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutafungua matumaini mapya kwa watu wa Pangani baada ya kutoa kilio chao kwa zaidi ya miaka 50.

    Ameomba kuwa sehemu kubwa ya ajira katika kazi za vibarua na huduma nyingine kama za chakula watu wa Pangani wapewe kipaumbele.

    Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutaleta matumaini mapya kwa mkoa wa Tanga ambapo itaunganisha kibiashara na mikoa ya kanda ya Kaskazini na Visiwa vya Unguja na Pemba.

    Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah Issa amesema kuwa mradi huo wa ujenzi ukikamilika utafungua fursa nyingine za kiuchumi na utalii nakuifanya Pangani kuwa ni kitovu cha kiuchumi na siyo njia ya kupitishia bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako