• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaipa Tanzania Milioni 217 kusaidia shughuli za kiofisi wakati wa mkutano wa SADC

  (GMT+08:00) 2019-08-16 09:44:22

  Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

  CHINA imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ofisini vyenye thamani ya zaidi ya milioni 217 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za ofisini wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa afrika (SADC).

  Tanzania inatarajia Kuwa mwenyeji wa mkutano Wa 39 wa Jumuiya hiyo unaofanyika mwezi huu tayari maandalizi yameanza ikiwemo maonesho ya viwanda huku kukifuatiwa na mikutano mbalimbali na Tanzania itapokea kijiti cha Uenyekiti Wa SADC Kutoka Kwa Namibia.

  Waziri wa mambo ya nje, Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, kikanda na Kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi amwaambia wanahabari Jijini Dar es Salaam kuwa wajasiriamali wanapaswa kuchangamkia mkutano huo ikiwemo Kompyuta, Mashine za photocopy na Printa kutoka kwa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya mkutano wa SADC.

  Mkutano Kama huu ulifanyika Tanzania Mara ya Mwisho mwaka 2003/2004 ambapo Rais wakati huo Benjamin Mkapa Alichaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa jumuiya Hiyo.

  Aipokea msaada huo, Waziri Kabudi alishukuru na kusema maandalizi ya shughuli za SADC yamekamilika kwa kiwango kikubwa na sasa Tanzania iko tayari kuanza kupokea wageni na viongozi waandamizi wa Nchi 16 wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

  Amesema maandalizi yamekamilika baada ya shughuli ya ukaguzi na kujiridhisha kuhusu utayari wa kuwapokea wageni na Serikali imejiridhisha kuwa ina uwezo na iko tayari kuwapokea wageni na viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika baada ya kukagua mahali watakapofikia,sehemu ya kufanyika kwa mikutano mbalimbali na mambo mengine muhimu kwa wageni hao.

  Anasema marais na wafalme wanatarajiwa kuanza kuwasili Agust 16 licha ya ukweli kuwa shughuli za SADC zimekwishaanza toka August 05, mwaka huu ambayo ilikuwa na wiki ya maonesho ya viwanda na siku ya maonesho hayo yalifungwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Shein ikifuatiwa na mkutano wa makatibu wakuu,mawaziri na kisha wakuu wa nchi na serikali ikijumuisha Marais na Wafalme.

  Katika mkutano huo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako