• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afisa ubalozi wa China ashauri vijana Tanzania kushiriki mchezo wa Wushu

    (GMT+08:00) 2019-08-16 09:45:57

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    MSIMAMIZI wa Kituo cha Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania Bw. Gao Wei ameshauri vijana wa Tanzania kushiriki katika mchezo wa Wushu akieleza kuwa itawasiadia kujijengea uwezo wa kujiamini na kushauri pia vyombo vya ulinzi kutumia mchezo huo kuwaongezea uzoefu zaidi .

    Wushu au Kungfu ya Kichina, ni mchezo wa upiganaji ulioanzishwa nchini China. Wushu umekuwa mchezo wa kimataifa kupitia Shiririkisho la Kimataifa la Wushu (IWUF - International Wushu Federation).

    Shirikisho hili ndilo huendeleza michezo ya kimataifa ya wushu kama vile Michuano ya Dunia ya Wushu inayofanyika kila baada ya miaka miwili tangu shindano la kwanza mwaka wa 1991 Beijing, China.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam mwisho wa wiki, Jumapili, Agosti 11, 2019, Bw. Gao aliongeza kuwa mafunzo ya mchezo wa Wushu yakitumiwa vizuri utakuwa msaada mkubwa kwa vijana wa Tanzania na Afrika kwa ujumla katika kuwakuza kinidhamu na kuwajengea ukakamavu.

    Bw. Gao alikuwa akishiriki katika sherehe za sita za kuwapa zawadi washindi wa mashindano ya kimataifa ya Wushu ambapo amesema kupitia mchezo huo vijana wengi wameweza kupata ajira katika sehemu mbalimbali.

    Naye Afisa Utamaduni Mkuu katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Habibu Msammy alisema kuwa mchezo wa Wushu Kungfu unawajengea vijana nidhamu na ukakamavu kwani ni moja ya mafunzo yaliyomo ndani ya mchezo huo pia inawapa fursa ya kwenda nje ya nchi ambapo hadi sasa vijana 70 wameshapatiwa mafunzo hayo nchini China.

    Pia amekipongeza chama cha Wushu kwa Kuanzisha kampuni ya ulinzi isiyotumia silaha na kuwasisitiza kuendeleza na kuanzisha miradi mingine na kuwa wabunifu ili wapata nafasi nyingi za kuajiri.

    Kwa upande wake Ofisa Upelelezi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Chief Kalimwoge amewashauri viongozi wa chama cha Wushu kuangalia namna ya kupeleka mchezo huo kwa nchi za Jumuiya ya Kusini Mwa Afrika SADC ili kuendeleza kuukuza mchezo huo Afrika.

    Amesema endapo mchezo huo utaendelea kupewa hamasa kubwa kwenye maeneo mengi utasaidia kutokomeza vitendo vya kihalifu na kuimarisha Afya kutokana na mafunzo hayo kutolewa kuanzia watoto wa shule za msingi na hatimaye Tanzania kuwa kitovu cha mchezo huo Afrika.

    Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Milinde Mahona alikitaka chama cha Wushu kuhakikisha kuwa kunakuwa na vituo vya mchezo huo kwa mikoa yote Tanzania ili vijana wengi wapate mbinu za kiulinzi na ajira tofauti na sasa ambapo wapo kwenye mikoa 11 tu na Baraza la Michezo milango iko wazi kwa msaada wowote watakaohitaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako