• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa samani za Ofisini kwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) huku Balozi wake akipongeza serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji

    (GMT+08:00) 2019-08-19 10:14:09

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    BALOZI wa China nchini Wang Ke amepongeza jitihada za serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kueleza kuwa mwaka huu mambo mengi yamefanyiwa kazi hivyo anatarajia wawekezaji zaidi nchini hususan kutoka nchini China.

    Alisema mbali na uboreshaji huo,Tanzania imekuwa sehemu nzuri ya uwekezaji kutokana na kuwa na soko la uhakika,nguvukazi, bandari hivyo kuwa na uhakika wa kusafirisha bidhaa kwa kuunganisha nchi mbalimbali na kubwa zaidi amani na utulivu uliopo kwa watu wake.

    Balozi alisema hayo jana wakati akitoa msaada wa samani za ofisi kwa ajili ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zanye thamani ya shilingi milioni 45 kuhakikisha kituo hicho kinahudumia vema wawekezaji.

    Balozi alisema katika masuala ya uwekezaji sera mbalimbali zimekuwa zikifanyiwa kazi lakini mwaka huu kumekuwa na kuondoa kodi na tozo mbalimbali zilizokuwa kero kwa wawekezaji hivyo kuongeza mazingira bora kwa wawekezaji nchini.

    Alisema China ikiwa nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini anaamini watakuja wawekezaji wengi zaidi hususan baada ya kukamilika kwa mpango wa ufanyaji biashara 'Blue Print' ikiwa ni fursa katika kuwezesha kuongeza viwanda nchini.

    Akizungumza wakati wa kupokea samani hizo, Mkurugenzi wa TIC, Geoffrey Mwambe alishukuru kwa msaada huo ambao amebainisha utasaidi katika uwekaji samani kwenye ofisi zao mpya hususan wa kupata ofisi mpya Dodoma.

    alisema samani walizopokea ni viti,meza,kabati na vinginevyo kwa ajili ya ofisi mpya watakayoamia hivi karibuni na kuomba wadau zaidi kuendelea kusaidia kituo hicho ili kuwahudumia wawekezaji .

    "katika hili,tuna mradi mkubwa pale Dodoma ya ujenzi wa ofisi ili kuwa karibu na serikali katika maamuzi mbalimbali kwani kwa sasa tupo Dar es Salaam ambao ni mji wa kibiashara ili kuwa karibu na wawekezaji"Alisema

    Alisema katika matumizi ya malighafi zilizopo nchini wamekuwa wakitengeneza samaki Magereza na tayari walitoa oda lakini walizopokea zimenunuliwa katika maduka ya samani kutokana na sababu mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako